KITUO
cha kurusha matangazo ya radio cha dini ya Kiislamu cha Alnoor
kimeteketea kwa moto ikiwemo studio zake tatu. Mkurugenzi mkuu wa Radio
Alnoor, Mohamed Suleiman Tall, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo
ambayo alisema chanzo chake kikubwa ni hitilafu ya moto katika kituo
kikuu cha umeme.
Alisema
moto huo ulianzia katika studio nambari tatu ambayo imeteketea huku
vifaa vyote ikiwemo kompyuta pamoja na vifaa vingine muhimu vya
mawasiliano ya redio vimeteketea.
"Radio Alnoor imeteketea kwa moto ambapo studio zake tatu zimeharibika na tunakisia tumepata hasara Sh milion 82," alisema.
Tall alisema juhudi za kiufundi za kurudisha matangazo ya Radio Alnoor hewani kwa wasikilizaji wake zinaendelea hadi sasa.
"Tunafanya
kila juhudi kuona kwamba wananchi wanapata matangazo ya Radio Alnoor,
licha ya kujitokeza kwa hitilafu kubwa ya studio zake kuteketea kwa
moto," alisema.
Kwa
mujibu wa maelezo ya mtangazaji mmoja Rashid Salum, alisema tukio hilo
limetokea majira ya saa nane za usiku huku chanzo kikubwa ni hitilafu za
umeme.
Mmoja
ya watangazaji wake Abubakar Fakih, amejeruhiwa kwa kuumia mguu baada
ya kuruka kutoka ghorofa ya pili kwa ajili ya kujihami na moto huo.
"Moto ulikuwa mkubwa kiasi nililazimika kujirusha kutoka ghorofa ya pili hadi chini kwa ajili ya kujiokoa," alisema Fakih.
Radio Noor ni maarufu visiwani hapa ambayo hurusha matangazo yake zaidi yenye muelekeo na kutoa Elimu ya dini ya Kiislamu
via>>eddy blog