Gari la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya mkoa wa Singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa.…
Gari la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya mkoa wa Singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa.
Moja ya maiti ya ajali ya basi la Sumry iliyotokea katika kijiji cha Utaho, Wilayani Ikungi mkoani Singida ikisubiri kupakiwa katika gari la polisi.
Watu 19 wa kijiji cha Utaho, wilayani Ikungi mkoani Singida wamepoteza maisha wakiwemo askari wanne wa jeshi la polisi, baada ya kugongwa na basi la Summry wakati wakiwa wanatoa msaada wa kumpakia marehemu kwenye gari la polisi aliyegongwa na gari kubwa ambalo halikufahamika mara moja jana usiku.
Basi hilo la kampuni ya Sumry hufanya safari zake kati ya Kigoma na Dar-es-Salaam.
Taarifa zinasema Dereva wa basi hilo alikimbia mara tu na baada ya ajali hiyo na kulitekeleza basi hilo.
Mwandishi wa habari Elisante Mkumbo alifika na kuwakuta wasafiri walionusurika wakiwa katika kituo cha polisi cha Ikungi bila ya kujua hatima yao ya safari baada ya basi lao kuwakanyaga na kuuwa watu 19.
Picha zote kwa hisani ya Elisante Mkumbo-ITV