KUHUSU TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO

DSC00361 “PRESS RELEASE” TAREHE 12.04.2014.
  • WATU 37 WAKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA FUJO NA KUHARIBU MALI.
 MTU MMOJA AKUTWA AMEJIUA CHUMBANI KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA WA NCHINI ETHIOPIA BAADA YA KUKAMATWA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

 KATIKA TUKIO LA KWANZA:
 WATU 37 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA FUJO NA KUHARIBU MALI.
 
 TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 11.04.2014 MAJIRA YA  SAA 10:30 ASUBUHI HUKO KATIKA ENEO LA IYELA – AIRPORT, KATA YA  IYELA,  TARAFA YA IYUNGA   JIJI NA   MKOA WA MBEYA AMBAPO KUNDI LA WATU WAKIWEMO WAENDESHA PIKIPIKI MAARUFU KWA JINA LA BODABODA ZAIDI YA  MIA MBILI WALIVAMIA KWENYE MSIBA WA MAREHEMU SIZA JOHN MWAMBENJA [28]  MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA AIRPORT  NA KUFANYA FUJO IKIWA NI PAMOJA NA KUHARIBU MALI MBALIMBALI KATIKA NYUMBA HIYO WAKISHINIKIZA KUMKAMATA MTALAKA WA MAREHEMU OLIVA HERODE MWAMLIMA [ 25] MKAZI WA FOREST MPYA AMBAYE ALIKUWEPO KATIKA MSIBA HUO KWA MADAI KUWA ANAHUSIKA NA NJAMA ZA MAUAJI YA  ALIYEKUWA MUME WAKE KUTOKANA NA KUACHWA KWA SABABU ZA MATATIZO YA KIFAMILIA.
 
 MAREHEMU SIZA JOHN MWAMBENJA ALIUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA MWILI WAKE KUKUTWA UMETUPWA KANDO YA RELI YA TAZARA  TAREHE 09.04.2014 UKIWA NA JERAHA LA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SHINGONI NA KANDO YAKE KUTELEKEZWA PIKIPIKI YAKE MPYA YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 932 CTZ AINA YA  KINGLION.
 
 KUFUATIA VURUGU HIZO ZILIZOZIMWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA, WATU 37 WALIKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMA YA MWANZO MBEYA MJINI AMBAO WALISOMEWA MASHITAKA YAO SHAURI LA JINAI NAMBA 291/2014. 
 
 WATUHUMIWA WOTE WAMEPELEKWA MAHABUSU GEREZA LA RUANDA AMBAPO KESI ITAANZA KUSIKILIZWA 14.04.2014.
 
AIDHA KATIKA VURUGU HIZO MALI ZA JESHI LA POLISI GARI MOJA LA KITUO CHA POLISI KATI  474 AINA YA  LAND ROVER 110  LILIHARIBIWA KWA KUPIGWA MAWE NA KUVUNJWA KIOO KIKUBWA CHA MBELE. 
 
HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA WAKATI WA VURUGU HIZO NA HALI YA AMANI ILIREJEA KUWA YA KAWAIDA NA WANANCHI WANAENDELEA NA SHUGHULI ZAO KAMA KAWAIDA.
 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE. 
 
AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUJENGA TABIA YA  KUHESHIMU MAMLAKA ZILIZOWEKWA KISHERIA IKIWA NI PAMOJA NA VYOMBO VYA DOLA ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA BADALA YA KULETA USHINDANI NA VURUGU. 
 
PIA KAMANDA MSANGI AMESISITIZA KUWA JESHI LA POLISI HALITASITA KUWAKAMATA NA KUWACHUKULIA HATUA KALI ZA KISHERIA WALE WOTE WANAOKAIDI NA KULETA VURUGU.
 
 KATIKA TUKIO LA PILI:
 MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JAIL RUBANGE [57] MKAZI WA WILAYA YA KYELA ALIKUTWA AMEJIUA KWA KUJICHOMA KISU SHINGONI KATIKA CHUMBA ALICHOPANGA.
 
 TUKIO HILO LIMETOKEA   HUKO KATIKA NYUMBA YA  KULALA WAGENI IITWAYO TEN COMMANDMENT ILIYOPO ENEO LA STENDI KUU KATA NA TARAFA YA  SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA TAREHE 11.04.2014 MAJIRA YA  SAA 10:30 ASUBUHI.
 
 CHANZO CHA TUKIO HILI BADO  KINACHUNGUZWA, INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI  UNAONYESHA MAREHEMU ALIKUWA ANASUMBULIWA NA MARADHI YA  KISUKARI NA BP KWA MUDA MREFU. 
 
MAREHEMU ALICHUKUA CHUMBA TAREHE 10.04.2014 MAJIRA YA  SAA 16:00 JIONI  NA ALIFANYA KITENDO HICHO BAADA YA   KUJIFUNGIA KWA NDANI KATIKA CHUMBA NAMBA 13 KISHA KUJIUA NA KISU. 
 
KISU ALICHOKITUMIA KIJIUA KILIKUTWA BADO KIPO SHINGONI. 
 
 AIDHA MAREHEMU HAKUACHA UJUMBE WOWOTE. MWILI WAKE ULIKUTWA NDANI KATIKA BAADA YA ASKARI POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WENYE NYUMBA KUVUNJA MLANGO.
 
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI INA MADHARA KWA JAMII.
 
 NA KATIKA TUKIO LA TATU:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI  1. LILE RAMA [20] NA 2. MESFIN HABTE [22] WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.  
 
WATU HAO WALIKAMATWA TAREHE 11.04.2014 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU KATIKA ENEO LA POSTA TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA  TUNDUMA WILAYA YA  MOMBA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI.
 
 TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAFANYIKA.
 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA  MSAIDIZI MWANDAMIZI  WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA  MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA NAA RAIA WA KIGENI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post