- WATU 37 WAKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA FUJO NA KUHARIBU MALI.
MTU MMOJA AKUTWA AMEJIUA CHUMBANI KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA WA NCHINI
ETHIOPIA BAADA YA KUKAMATWA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU 37 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA FUJO NA KUHARIBU MALI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 11.04.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI HUKO
KATIKA ENEO LA IYELA – AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA JIJI
NA MKOA WA MBEYA AMBAPO KUNDI LA WATU WAKIWEMO WAENDESHA PIKIPIKI
MAARUFU KWA JINA LA BODABODA ZAIDI YA MIA MBILI WALIVAMIA KWENYE MSIBA
WA MAREHEMU SIZA JOHN MWAMBENJA [28] MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA,
MKAZI WA AIRPORT NA KUFANYA FUJO IKIWA NI PAMOJA NA KUHARIBU MALI
MBALIMBALI KATIKA NYUMBA HIYO WAKISHINIKIZA KUMKAMATA MTALAKA WA
MAREHEMU OLIVA HERODE MWAMLIMA [ 25] MKAZI WA FOREST MPYA AMBAYE
ALIKUWEPO KATIKA MSIBA HUO KWA MADAI KUWA ANAHUSIKA NA NJAMA ZA MAUAJI
YA ALIYEKUWA MUME WAKE KUTOKANA NA KUACHWA KWA SABABU ZA MATATIZO YA
KIFAMILIA.
MAREHEMU
SIZA JOHN MWAMBENJA ALIUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA MWILI WAKE
KUKUTWA UMETUPWA KANDO YA RELI YA TAZARA TAREHE 09.04.2014 UKIWA NA
JERAHA LA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SHINGONI NA KANDO YAKE
KUTELEKEZWA PIKIPIKI YAKE MPYA YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 932 CTZ AINA
YA KINGLION.
KUFUATIA VURUGU HIZO ZILIZOZIMWA NA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA, WATU 37 WALIKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMA YA MWANZO MBEYA
MJINI AMBAO WALISOMEWA MASHITAKA YAO SHAURI LA JINAI NAMBA 291/2014.
WATUHUMIWA WOTE WAMEPELEKWA MAHABUSU GEREZA LA RUANDA AMBAPO KESI
ITAANZA KUSIKILIZWA 14.04.2014.
AIDHA
KATIKA VURUGU HIZO MALI ZA JESHI LA POLISI GARI MOJA LA KITUO CHA
POLISI KATI 474 AINA YA LAND ROVER 110 LILIHARIBIWA KWA KUPIGWA MAWE
NA KUVUNJWA KIOO KIKUBWA CHA MBELE.
HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU
YALIYORIPOTIWA KUTOKEA WAKATI WA VURUGU HIZO NA HALI YA AMANI ILIREJEA
KUWA YA KAWAIDA NA WANANCHI WANAENDELEA NA SHUGHULI ZAO KAMA KAWAIDA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA
WATUHUMIWA WANOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI HATUA ZA KISHERIA
DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUJENGA TABIA YA
KUHESHIMU MAMLAKA ZILIZOWEKWA KISHERIA IKIWA NI PAMOJA NA VYOMBO VYA
DOLA ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA BADALA YA KULETA
USHINDANI NA VURUGU.
PIA KAMANDA MSANGI AMESISITIZA KUWA JESHI LA POLISI
HALITASITA KUWAKAMATA NA KUWACHUKULIA HATUA KALI ZA KISHERIA WALE WOTE
WANAOKAIDI NA KULETA VURUGU.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MFANYABIASHARA
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JAIL RUBANGE [57] MKAZI WA WILAYA YA
KYELA ALIKUTWA AMEJIUA KWA KUJICHOMA KISU SHINGONI KATIKA CHUMBA
ALICHOPANGA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA HUKO KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI IITWAYO TEN
COMMANDMENT ILIYOPO ENEO LA STENDI KUU KATA NA TARAFA YA SISIMBA JIJI
NA MKOA WA MBEYA TAREHE 11.04.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI.
CHANZO
CHA TUKIO HILI BADO KINACHUNGUZWA, INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI
UNAONYESHA MAREHEMU ALIKUWA ANASUMBULIWA NA MARADHI YA KISUKARI NA BP
KWA MUDA MREFU.
MAREHEMU ALICHUKUA CHUMBA TAREHE 10.04.2014 MAJIRA YA
SAA 16:00 JIONI NA ALIFANYA KITENDO HICHO BAADA YA KUJIFUNGIA KWA
NDANI KATIKA CHUMBA NAMBA 13 KISHA KUJIUA NA KISU.
KISU ALICHOKITUMIA
KIJIUA KILIKUTWA BADO KIPO SHINGONI.
AIDHA MAREHEMU HAKUACHA UJUMBE
WOWOTE. MWILI WAKE ULIKUTWA NDANI KATIKA BAADA YA ASKARI POLISI KWA
KUSHIRIKIANA NA WENYE NYUMBA KUVUNJA MLANGO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI KWANI INA MADHARA KWA JAMII.
NA KATIKA TUKIO LA TATU:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. LILE RAMA [20]
NA 2. MESFIN HABTE [22] WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA
WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WATU
HAO WALIKAMATWA TAREHE 11.04.2014 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU KATIKA ENEO
LA POSTA TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA KUFUATIA
MSAKO ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI.
TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAFANYIKA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE IKIWA NI PAMOJA NAA RAIA WA KIGENI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.