Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUTANA NA MCHUNGAJI HUYU WA KANISA ANAYEDAI HAWAJAHI KUOGA TANGU 2001,ADAI ALIAMBIWA NA MUNGU ASIOGE



Nadhani ulishawahi kusikia ama kushuhudia watu wa eneo Fulani ama jamii fulani wakimlazimisha kichaa kuoga kwa nguvu kwa kuwa amezidi kuwa mchafu, lakini hii ni tofauti kwa waumini wa dhehebu analolisimamia mchungaji Wale Olanguji wa Nigeria.
 

Mchungaji Wale wa kanisa la Divine Seed of God wa Ibadan, Oyo, Nigeria ameliambia jarida la People City la Nigeria kuwa hajawahi kuoga tangu mwaka 2001 wakati ambapo anadai alipokea amri ya Mungu ikimtaka afanye hivyo na kwamba ajitenge na mkewe na kuacha kutumia baadhi ya vinywaji.


 
Cha ajabu, licha ya kukaa miaka 13 bila kuoga mchungaji huyo hatoi harufu na ni vigumu kumshitukia hadi akuoneshe mwenyewe vielelezo!


 
Hivi ndivyo mchungaji huyo alivyoliambia jarida hilo wakati lilipomkumbusha kuwa mwaka 2001 alitoa maelezo kuwa Mungu amemwambia asioge:


 
"Ndiyo, ni miaka 13 hadi sasa kwa ufupi. Mwaka 2000 mwanzoni Mungu aliniambia niache kuoga, nijitenge na mke wangu na kwamba natakiwa kuacha kutumia vinywaji vyote laini pamoja na wines. Na tangu wakati huo…kwa kweli, nimekuwa nikifuata yote hayo. 


 
"Mtu yeyote ambaye Mungu anataka kumtumia kwa sababu hapa duniani, kuna gharama imeambatanishwa kwenye huo wito. Kwa hiyo ninaamini kwamba hiyo ni gharama ninayolipa. Ninavyoongea na wewe hivi sasa, sijaoga, kama unataka nikuoneshe ushahidi nitakuonesha kama una shaka juu ya haya yote nisemayo; sijaoga tangu mwaka 2001 hadi wakati huu."




>>Times 100.5 fm 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com