Mkuu wa wilaya ya Nyang'wale Ibrahim Malwa akitoa heshima za mwaisho kwa marehemu |
Mhashamu askofu Damian Dallu wa
jimbo la Geita leo ameongoza ibada ya misa ya kumuombea na
kumuaga marehemu padri Henry Kimisha aliyekuwa paroko wa parokia ya
kanisa la mama fatima lililopo mjini Geita aliyefariki dunia ghafla mwezi huu kwa
shinikizo la damu.
Akiongoza
ibada hiyo leo iliyofanyika katika kanisa kuu jimbo la Geita Damiani
Dallu ambayo pia imehudhuriwa na askofu Marco Msonganzila kutoka jimbo la Musoma na askofu Renatus Nkwande wa jimbo la Bunda askofu Dallu amesema amewataka waumini kuiga mambo yote mazuri aliyoyafanya Padri
Kimisha katika uhai wake huku akiwataka kujiandaa wakati wote kwani haijulikani siku wala saa ya kufa.
Mhashamu askofu Damian Dallu amesema ni vyema wakristo wote wakajiandaa kwa kuwasaidia
wahitaji na wajane na wenye shida mbalimba wangali wako hai akatoa mfano kuwa
Kimisha aliwasaidia watu wengi wahitaji na wenye shida mbalimbali hivyo kuwataka
wakristo kuiga mfano wake.
Amesema Padri Kimisha atakumbukwa kwa mambo mengi aliyoyafanya katika
parokia ya Geita kubwa ikiwa ni kuwahimiza vijana na wazee kufunga ndoa kuliko kukaa
katika maisha ya kishetani.
Padiri
Kimisha alizaliwa tarehe 8. 6. 1967 katika kijiji cha Katunguru wilaya ya Sengerema
mkoa wa Mwanza na alipata daraja la upadri tarehe 25 .7. 1996 katika parokia ya
Nyantakubwa Sengerema mkoa wa Mwanza na alifariki siku ya jumatatu kwa shinikizo
la damu katika hositari ya wilaya Geita na amezikwa leo kati makaburi ya kanisa
la mama wa Fatima yalioko katika kanisa hilo.
Mazishi ya padri Kishisha yamehudhuriwa pia na viongozi wa serikali wakiwemo naibu waziri wa
mawasiliano na uchukuzi Dk,Charles Tizeba mkuu wa mkoa wa Mwanza
Dk,Evarist Ndikilo na mkuu wa wilaya ya Geita Omari Mangochie,mkuu wa
wilaya ya Nyang'hwale Ibrahimu Marwa na mkuu wa wilaya ya Ngara
Costantine Kanyasu pamoja na mapadri,masisita,
waumini na watu wenye mapenzi mema kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita na mikoa jirani.
Mungu ailaze mahala pema mbinguni roho ya marehemu padri Kishisha.Amina!!
waumini na watu wenye mapenzi mema kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita na mikoa jirani.
Mungu ailaze mahala pema mbinguni roho ya marehemu padri Kishisha.Amina!!
Na Valence Robert-Geita.
Social Plugin