Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla |
Wakati wakristo na watu mbalimbali wenye mapenzi mema kote
duniani wakiendelea kusherehekea sikukuu ya pasaka hali imekuwa tofauti katika familia
ya bwana Stephen Philbert(30) mkazi wa Ngokolo mjini Shinyanga kufuatia kuuawa kwake kwa kuchomwa kisu wakati
akifanya jaribio la kumbaka mwanamke mmoja (jina tunalo mwenye umri wa miaka 24)katika
eneo la Ngokolo mjini Shinyanga usiku wa mkesha wa pasaka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist
Mangalla ameuambia mtandao huu wa malunde1 blog kuwa tukio hilo limetokea Aprili 20 ,mwaka huu saa tisa usiku.
Amesema siku ya
tukio mwanamme huyo alivunja dirisha la nyumba ya mwanamke huyo na kuingia
ndani kisha kufanya jaribio la kumbaka lakini katika kujihami kwake ndipo mwanamke huyo alimchoma kisu
kichwani ,akafariki dunia akiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano
zaidi.
Social Plugin