Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Majanga ya Pasaka Shinyanga- JAMAA ACHOMWA KISU NA MWANAMKE,ALIVUNJA DIRISHA NA KUTAKA KUMBAKA MWANAMKE HUYO

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla
Wakati wakristo na watu mbalimbali wenye mapenzi mema kote duniani wakiendelea kusherehekea sikukuu ya pasaka hali imekuwa tofauti katika familia ya bwana Stephen Philbert(30) mkazi wa Ngokolo mjini Shinyanga kufuatia  kuuawa kwake kwa kuchomwa kisu wakati akifanya jaribio la kumbaka mwanamke mmoja (jina tunalo mwenye umri wa miaka 24)katika eneo la Ngokolo mjini Shinyanga usiku wa mkesha wa pasaka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla ameuambia mtandao huu wa malunde1 blog kuwa tukio hilo limetokea Aprili 20 ,mwaka huu saa tisa usiku.

Amesema  siku ya tukio mwanamme huyo alivunja dirisha la nyumba ya mwanamke huyo na kuingia ndani kisha kufanya jaribio la kumbaka lakini katika kujihami kwake ndipo mwanamke huyo alimchoma kisu kichwani ,akafariki dunia akiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com