Katika hali isiyo kawaida mwanafunzi wa kidato
cha kwanza aliyetajwa kwa jina moja la Musa anadaiwa kuwabaka wanafunzi
watatu wa shule ya msingi hadi kuwaharibu sehemu za siri.
Tukio hilo la karne lilitokea Kigogo-Luhanga jijini Dar ambapo denti
huyo wa sekondari anayeishi na bibi yake aliwabaka watoto hao wanaosoma
darasa la kwanza, la pili na la tatu.
Wakizungumza kwa huzuni na kwa nyakati tofauti, wazazi
wa watoto hao walisema waligundua ukatili huo baada ya kaka wa mtoto
mmojawapo kumbana mdogo wake ambapo alieleza jinsi mwanafunzi huyo
alivyokuwa akiwafanyia kitendo hicho kwenye banda la kuku wakati watu
wamekwenda kwenye shughuli zao.
Akizungumza na Amani, mama wa mtoto mmoja alisema:
“Imeniuma sana, mara nyingi mwanangu anaoga mwenyewe kwa sababu mimi nakuwa kwenye biashara, nakosa muda wa kumkagua ndiyo maana huyu kijana alipata nafasi ya kumharibu kiasi hiki.”
“Imeniuma sana, mara nyingi mwanangu anaoga mwenyewe kwa sababu mimi nakuwa kwenye biashara, nakosa muda wa kumkagua ndiyo maana huyu kijana alipata nafasi ya kumharibu kiasi hiki.”
“Bila yule kijana kumshtukia mdogo wake aliyekuwa akitembea kama vile
alikuwa ameumia hivyo kupata maumivu, ingetuchukua muda mrefu kubaini
kama walifanyiwa kitendo kibaya,” alisema mama huyo.
Mama mwingine ambaye aliomba hifadhi ya jina lake alisema, amehuzunishwa sana na kitendo ambacho Musa amewafanyia watoto wao.
Aliongeza kuwa, kwa jinsi alivyo kijana huyo huwezi kudhania anaweza kufanya kitendo cha kinyama kama alichowafanyia watoto wao.
“Kwakweli nikiwa kama mzazi nimeumia sana naomba sheria ichukue
mkondo wake ili iwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia kama hiyo
isiyofaa kwenye jamii,” alisema mama huyo.
Mzazi mwingine wa kiume ambaye mtoto wake ni miongoni mwa waliobakwa (jina lake tunalihifadhi), amelaani sana kitendo hicho.
Mzazi mwingine wa kiume ambaye mtoto wake ni miongoni mwa waliobakwa (jina lake tunalihifadhi), amelaani sana kitendo hicho.
“Binafsi kitendo alichokifanya kijana huyo kimenikera mno kwa sababu
kitawafanya watoto wetu kutosahau unyama huo katika maisha yao yote,”
alisema mzazi huyo.
Watoto hao walikiri kufanyiwa kitendo hicho na Musa kwenye banda la kuku, siku nyingine chumbani kwake.
Watoto hao walikiri kufanyiwa kitendo hicho na Musa kwenye banda la kuku, siku nyingine chumbani kwake.
Wazazi hao walitoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Kigogo- Luhanga na
kupewa jalada la kesi MBL/RB/198/2014, MBL/RB/199/2014 KUBAKA. Mtoto
mmoja, mzazi wake alichelewa kwenda kufungua shauri.
Mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni Musa alikuwa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Urafiki, Ubungo jijini Dar.
Na Gladness Mallya na Deogratius Mongela
Social Plugin