NB-Picha haiendani na stori |
Mahakama moja ya kiisilamu katika jimbo la Kano nchini Nigeria, imemkuhuku kifo mzee mwenye umri wa miaka 60 kwa kupigwa mawe hadi afe baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 12.
Mwanamume huyo pia aliripotiwa kumuambukiza msichana huyo virusi vya HIV.
Hukumu kama hizi hutolewa chini ya sheria kali za kiisilamu na zimewahi kupitishwa ingawa utekekelezaji wake unakuwa mgumu.
Hukumu ambazo ziliwahi kutolewa hapo awali ziligeuzwa na kuwa kifungo cha maisha jela.
Mtuhumiwa Ubale Sa'idu Dotsa, alijitetea mahakamani Jumatano, akisema kuwa shetani ndiye aliyemsababisha kumbaka msichana huyo.
Alisema hakujua kama alikuwa ameambukizwa virusi vya HIV.
Dotsa alisema kuwa msichana huyo alimfanya kupata hisia alipotembelea duka lake mara kwa mara nyakati za usiku na ndio maana akambaka.
Hakimu Faruk Ahmed, alipuuza kilio cha mzee huyo aliyetaka mahakama kumsamehe.
Alisema mzee huyo kwa jina Dotsa alikuwa ametenda zinaa, kitendo ambacho adhabu yake ni mtu kuuawa kwa kupigwa mawe.
via>>BBC
Social Plugin