TAZAMA KIJANA HUYU ALIVYOJERUHIWA NA MAJAMBAZI HUKO TABORA,YADAIWA WANAVAMIA KILA SIKU USIKU
Tuesday, April 01, 2014
Salumu
Abel Muhunda mkazi wa Kata ya Cheyo manispaa ya Tabora amejeruhiwa
vibaya na kundi la Majambazi ambayo yalimvamia wakati akiuza dukani
huko eneo la Mwanga Shop ambapo majambazi hayo yalivamia yakiwa na
bunduki na kufyatua risasi hewani huku yakimjeruhi kwa kumpiga mapanga
na nyundo kichwani na baadae kumpora kiasi kikubwa cha fedha.
Salumu
Abel Muhunda
ambaye kwa sasa amelazwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ni
mmoja kati ya watu walioathirika na matukio ya unyang'anyi wa kutumia
silaha unaofanywa na majambazi hayo ambayo hufanya unyama huo kila siku
na kwasasa takribani miezi mitatu mfululizo eneo la manispaa ya Tabora
waathirika wakubwa ni wafanyabishara ya maduka madogo ya mitaani pamoja
na M-pesa.PICHA KWA HISANI YA KAPIPIJ BLOG
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin