Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAZAMA KIJANA HUYU ALIVYOJERUHIWA NA MAJAMBAZI HUKO TABORA,YADAIWA WANAVAMIA KILA SIKU USIKU

Salumu Abel Muhunda mkazi wa Kata ya Cheyo manispaa ya Tabora amejeruhiwa vibaya na kundi la Majambazi ambayo yalimvamia wakati akiuza dukani  huko eneo la Mwanga Shop ambapo majambazi hayo yalivamia yakiwa na bunduki na kufyatua risasi hewani huku yakimjeruhi kwa kumpiga mapanga na nyundo kichwani na baadae kumpora kiasi kikubwa cha fedha.
Salumu Abel Muhunda  ambaye kwa sasa amelazwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ni mmoja kati ya watu walioathirika na matukio ya unyang'anyi wa kutumia silaha unaofanywa na majambazi hayo ambayo hufanya unyama huo kila siku na kwasasa takribani miezi mitatu mfululizo eneo la manispaa ya Tabora waathirika wakubwa ni wafanyabishara ya maduka madogo ya mitaani pamoja na M-pesa.PICHA KWA HISANI YA KAPIPIJ BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com