Matukio ya wananchi kuendelea kujichukulia sheria mkononi limeendelea kushika kasi mkoani Shinyanga ambapo huko katika kijiji na kata ya Busoka wilaya ya
Kahama kijana mmoja ameuawa kikatili kwa kushambuliwa kwa silaha za jadi kisha kuchomwa moto baada
ya kuiba ng’ombe wa baba yake mzazi.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla amesema tukio hilo limetokea Aprili 8,mwaka huu saa tisa alasiri,ambapo wananchi waliojichukulia sheria mkononi kumshambulia kwa silaha za jadi kisha mwili wake kuuchoma moto.
Kamanda Mangalla amemtaja kijana huyo kuwa ni Shida
Petro(17) mkazi wa Bugarama wilayani Kahama ambaye ameuawa kikatili kwa
kushambuliwa kwa silaha za jadi kisha mwili wake kuchomwa baada ya kumtuhumu kuiba ng’ombe
watatu wa baba yake mzazi aitwaye Petro Sangashelile ambao
walimkuta nao na kuanza kumshambulia na kusababisha kifo chake. .
Tayari jeshi la polisi linawanawashikilia
watu tisa kuhusiana na tukio hilo.
Social Plugin