Mauza uza,Uchawi!! CHUNGU CHA AJABU CHAIBUKA JUU YA KABURI KIKIFOKA DAMU,NI KWENYE KABURI LA MTOTO ALIYEFARIKI KIMIUJIZA HUKO IRINGA

Hivi ndivyo  vilivyokuwemo ndani na damu ,maini na kichwa cha ndege
Chungu  cha ajabu  kilichokutwa juu ya kaburi  katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa  leo kikiwa  kinafoka  damu
Wananchi  wakishuhudia chungu  hicho cha ajabu  kushoto  karibu na jembe na hapo ndipo kilipoibukia
Baba wa mtoto Agnes Mlawa akichimbua chungu  hicho
Baba  wa mtoto huyo kulia akisaidiwa na msamalia  mwema  kufungua chungu hicho ili kuona ndani

Hapa msamaria  mwema  akionyesha vitu  vilivyopo ndani
Tunguli ikiteketezwa  kwa moto
Mauza  uza matupu  kaburi  la mtoto Agnes Mlawa (8) mkazi  wa Ilala  katika Manispaa ya  Iringa aliyezikwa mwaka  jana na leo baba  wa  mtoto  huyo kakuta chungu cha ajabu chenye damu,maini na kichwa cha ndege kimechimbiwa  kaburini.

Tukio  hilo la aina  yake  limetokea leo majira ya saa 2 asubuhi  katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa wakati  baba mzazi wa mtoto  huyo Bw. Mlawa  wakati  akichembua kaburi  hilo na mara  baada ya  kumaliza  ghafla alishuhudia tukio hilo la chungu  cha ajabu  kuibuga juu ya kaburi  hilo .

" mimi hapa leo  nilikuja  kusembua  kaburi la mwanangu  ila  baada ya  kumaliza  ghafla  nilikuta kama damu  zinaruka juu  kutoka kaburini na baada ya  kuchunguza  ndipo nilipoona  chungu hicho kikiibuka juu ya kaburi "

Alisema  kuwa chungu  hicho kilikuwa  kimefungukwa na kitambaa cheusi juu ambacho  kimelowa  dawa  na kufungwa kamba ya  nguo ya  kijani  na kutokana na  tukio hilo la ajabu alilazimika  kuacha jembe  juu ya kaburi na kukimbia  kuita  watu  wanaopita barabarani  ili  kuomba msaada zaidi.

Mzazi   huyo anadai kuwa  mazingira ya kifo cha mtoto  wake  yalikuwa ni ya kushangaza  baada ya  kuugua kwa  muda wa  siku  nne pekee na kufariki  dunia .

Hata  hivyo  alisema  kwa  kuwa kwa upande  wake haamini mambo ya kishirikiana  hakuona  sababu  ya  kumwita  mganga  wa  kienyeji kwa ajili ya  kushughulikia  kuchoma chungu  hicho na badala  yake  kuamua  kuifanya kazi  hiyo mwenyewe hasa  akiamini nguvu ya Mungu  zaidi.

" Napenda  kuwashukuru  wananchi  waliofika  hapa kwa kunitia  nguvu na  pia kuwashukuru madereva  boda  boda  akiwemo kijana  Ahmed kwa  kujitolea  mafuta  ya Petrol kwa  ajili ya kukichoma chungu  hiki "

Mbali ya  mzazi   huyo  kujitolea  kuchuma chungu  hicho na kuteketeza  vitu vilivyo kuwemo ndani wananchi  waliofika  kushuhudia  tukio  hilo  walilazimika  kutimua  mbio  kuhofu zoezi hilo la uchomaji wa  tunguli  hizo.
Via>>matukiodaima.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم