Mfano wa kuigwa!!-PSPF YASHUSHA NEEMA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU SHINYANGA,YATOA ZAWADI KWA WATOTO WENYE ULEMAVU
Wednesday, April 30, 2014
Hapa ni katika ukumbi uliopo katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(albino)wasiosikia na wasioona kilichopo eneo la Buhangija mjini Shinyanga,ambacho sasa kina watoto 260,wa kiume 134 na wa kike 126.Watoto hao ambao wanadai kutelekezwa na wazazi na walezi wao. Leo mfuko wa pensheni wa PSPF (Public Service Pension Fund), umewapatia zawadi ya mabegi ya kubebea madaftari,madaftari,kalamu na kompasi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni mbili
Aliyesimama ni afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga aliyekuwa ameambatana na meneja wa kumbukumbu wa mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka makao makuu jijini Dar es salaam Chacha Nyaikwabe, akizungumza katika kituo hicho ambapo alisema PSPF imeona vyema kufika katika kituo hicho kutokana na kuwa wadau wakubwa wa elimu hapa nchini
Wa kwanza kushoto ni mwalimu Edward Mdagata ambaye ni afisa elimu maalum manispaa ya Shinyanga kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga idara ya elimu manispaa,wa pili ni meneja wa kumbukumbu wa mfuko wa Pensheni wa PSPF Chacha Nyaikwabe, wa kwanza kutoka kulia ni afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga wa pili kutoka kulia ni mkuu wa shule ya Buhangija jumuishi Peter Ajali.
Meneja wa kumbukumbu wa mfuko wa Pensheni wa PSPF Chacha Nyaikwabe akizungumza katika kituo hicho cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija ambapo alisema PSPF inajali sana elimu,na mara nyingi imekuwa ikitoa misaada katika vyuo mbalimbali lakini sasa imeamua kurudi kwenye shule za msingi ambako ndiko msingi wa elimu na leo wamefika katika kituo hicho kutoa zawadi yaya mabegi ya kubebea madaftari,madaftari,kalamu na kompasi vyote vikiwa na thamani ya milioni mbili kwa watoto hao.Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka watoto hao kusoma kwa bidii,huku akiwaasa kwamba kuwa na ulemavu haimaanishi kuwa wakose haki ya elimu
Watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasioona na wasiosikia wakimsikiliza Meneja wa kumbukumbu wa mfuko wa Pensheni wa PSPF Chacha Nyaikwabe
Aliyesimama ni mwalimu Edward Mdagata ambaye ni afisa elimu maalum manispaa ya Shinyanga kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga idara ya elimu manispaa akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo aliyataka mashirika na watu binafsi kufika katika kituo hicho kwani watoto wanafurahi kuona jamii inawajali pamoja na kwamba wazazi na walezi wamewatelekeza watoto hao
Watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija ambacho ndio kituo kikubwa nchi nzima wakichukua mabegi ya kubebea madaftari,madaftari,kalamu na kompasi kutoka kwenye gari la mfuko wa pensheni wa PSPF (Public Service Pension Fund) mara baada ya afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga pamoja na meneja wa kumbukumbu PSPF makao makuu wakiwa wameambatana na waandishi wa habari kuwasili eneo hilo
Watoto wakiendelea na zoezi la kuchukua mizigo kutoka kwenye gari la PSPF
Meneja wa kumbukumbu wa mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka makao makuu jijini Dar es salaam Chacha Nyaikwabe akikabidhi zawadi kwa watoto hao
Mtoto akifurahia zawadi kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii PSPF
Watoto wenye ulemavu wakipiga makofi kuushukuru mfuko wa pensheni wa PSPF kwa kuwajali,pamoja na kwamba wanakabiliwa na changamoto nyingi kama vile uhaba wa mabweni na vitanda na upungufu wa madawati ambapo sasa baadhi wanalazimika kukaa chini wakiwa darasani
Aliyesimama ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Buhangija Peter Ajali akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo kutoka PSPF ambapo alieeleza kufurahishwa na hatua iliyofanywa na PSPF kuwafikia watoto wenye ulemavu huku akiyataka mashirika na watu binafsi wenye mapenzi mema kuona umuhimu wa kufika katika kituo hicho na kuwasaidia watoto hao
Aliyesimama ni mtoto mwenye ulemavu wa kutoona Daniel Limbu anayesoma darasa la sita ambaye ni kiranja wa taaluma katika shule hiyo,akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi ambapo aliiomba serikali,mashirika na watu wenye mapenzi mema kuendelea kuwasaidia na mungu atawasaidia.Hata hivyo alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya vitendea kazi(vifaa maalum kwa watu wenye ulemavu)
Meneja wa kumbukumbu wa mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka makao makuu jijini Dar es salaam Chacha Nyaikwabe na Aliyesimama ni afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija mjini Shinyanga
Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga akiwa ambeba mmoja wa watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo hicho cha Buhangija
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin