MKUU WA KITUO CHA POLISI KAHAMA AGONGA WATU WATATU KWA GARI,YADAIWA ALIKUWA AMELEWA,MAJERUHI WAKO HOI ,TAZAMA PICHA HAPA

Majeruhi wa awali Joseph Malugu akiwa hospitali ya wilaya ya Kahama baada ya kuumia vibaya mguu wake na sehemu zingine za mwili.
 

Msukuma Toroli Fitina Majuto akiwa katika Hospitaliya wilaya ya Kahama
Mtembea kwa miguu Cosmas Peter akiwa hoi hospitalini
Mkuu wa kituo cha Polisi Kahama Elias Haway
Watu watatu  wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani shinyanga kufuatia ajali ya kugongwa na gari iliyokuwa ikiendeshwa na mkuu wa kituo cha polisi cha wilaya ya Kahama Elias Haway huku mmoja akiwa ameumia vibaya sehemu ya mguu.

Ajali hiyo imetokea Jana majira ya 1.30 usiku katika barabara itokayo isaka kuingia kahama mjiniu ambapo Haway akiendesha gari yake Toyota  Rav 4  lenye namba T 798  BSK alimgonga mwendesha pikipiki.

Watu waliogongwa wametambuliwa kwa majina ya Joseph Malugu (35) mkazi wa Mbulu  Bw. Fitina Majuto (20) na Cosmas Peter (21) wote wakazi wa mtaa wa  Nyasubi mjini Kahama.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Haway alianza kumgonga mwendesha bodaboda Bw. Malugu katika eneo la Zahanati ya Igalilimi  ambapo watu  wenye hasira  walimzingira wakimtaka asimame naye akakimbia huku akiwagonga tena  waenda kwa mguu wawili.

Wamesema Haway alionekana kuwa amelewa hakutaka kuwatii  watu  waliokuwa wakimweleza  ndipo alipoondoa  gari lake   kwa mwendo kasi   na  kwenda kumgonga   Majuto katika   eneo la  Mkude  ambaye aliumia vibaya kwenye sehemu ya tumbo na kusababisha utumbo kutoka nje.

Wamesema  baada ya kuondoa gari eneo Haway hakutaka kusimama na aliendelea na mwendo kasi ndipo alipokwenda kumgonga mtu mwingine  wa tatu   Peter katika barabara  ya eneo la Paradise mitaa ya Nyasubi.
  
Haway alipohojiwa amekiri kutokea kwa ajali hiyo na kudai kuwa kuna upotoshaji mkubwa wa taarifa hiyo kwani yeye ndiye aliyegongwa na mwendesha pikipiki huyo wa kwanza.

Amesema alipotaka kusimama kumwona mtu huyo aliyegonga,  aliona watu wameanza kumzonga naye akaamua kukimbia kwa usalama wake ndipo alipoweza kuwagonga tena wale wengine wawili.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Kahama Dk Joseph Foma amethibitisha kugongwa na gari watu hao na wamelazwa katika wodi namba moja katika hospital hiyo, huku hali zao zikiwa mbaya na kwamba wapo katika utaratibu wa kumuhamishia Malugu katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza.
Via>> Farajimfinanga.info

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post