Mwanafunzi
wa shule ya Sekondari Nandanga wa kidato cha kwanza Lukas Msukwa
amefariki dunia baada ya kutumbukia katika shimo la Maji lililochimbwa
na watengeneza barabara ya Mpemba hadi Wilayani Ileje, Mkoani Mbeya.
Tukio
hilo limetokea juzi majira ya saa saba mchana katika Kijiji cha
Nandanga, wilaya ya Momba ambapo inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni
baada ya marehemu kuteleza na kutumbukia katika shimo hilo lenye urefu
wa kina kati ya futi 20 na zaidi ambalo lilikuwa na maji.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed
Msangi ametoa wito kwa jamii kufunika pamoja na kufukia mashimo yaliyo
wazi kwa kuwa ni hatari kwa watoto na hata watu wazima.
Social Plugin