Mwenyekiti wa CCM UK Ndugu
Maina Ang'iela Owino jana ametangaza rasmi nia yake ya kujiuzulu Uongozi wa
CCM Tawi la UK
baada ya kutumikia toka mwaka 2007.
Ndugu
Owino alitoa uamuzi huo
wa hiari wakati akifungua rasmi kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Tawi la
UK kilichokaa Jumamosi tarehe 12/04/2014 katika jiji la Reading,
Berkshire,
Uingereza.
Ndugu Owino aliwakumbusha
wajumbe kuwa awali aliomba kukitumikia Chama kwa muhula mmoja wa uongozi na
alitaja kumbukumbu ya vikao vya Chama vilivyomuomba aendelee kukisimamia Chama
hasa baada ya kuchaguliwa viongozi wakuu wapya wa Tawi mwezi septemba 2012 jijini Manchester.
Ndugu Owino aliwakumbusha
mafanikio waliyopata katika muda wa uongozi wake ikijumuisha harakati za
kufungua mashina hadi 15 katika miji na Jiji mbalimbali; Kuhamasisha na kujenga
mtandao wa kuanzisha Jumuiya ya kwanza ya Watanzania hapa UK na Kuwashirikisha wanaCCM kuanzisha miradi ya
kujitegema ikiwepo ari ya kumiliki jengo la CCM UK.
Alikumbusha pia juhudi na
msukumo wa kutaka CCM Taifa kuanzisha dawati rasmi la matawi ya nje na kuyapa
uwakilishi wa kudumu katika vikao vya juu vya CCM Taifa.
Pia kupigania Sera ya
CCM ya Diaspora iboreshwe kwa Kuanzisha Kituo Maalum cha Diaspora nchini Tanzania ili
serikali iwashirikishe na kuratibu hoja na haja za wana Diaspora.
Aidha aliwataka wajumbe kutoa
ushirikiano wa wazi kwa Idara ya uenezi ambayo kwa sasa inajenga Website ya
kisasa na Online TV itakayowapa wanaCCM uhuru wa kutoa maoni na hoja zao bila
uwoga lakini kwa nidhamu na kufungua soko la kutangaza bidhaa za Tanzania.
Ndugu Owino alisema wanaCCM
hujenga umoja wa kweli na hawaogopi kusingiziwa au kusemwa vibaya na hivyo
wasiogope changamoto mbalimbali wakati wanatekeleza Mapinduzi ya umma na
kukijenga Chama hapa Uingereza.
Ndugu Owino aliiomba
Halmashauri Kuu ya Tawi ishirikiane na Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Tawi
kufanya maandalizi na kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu wakati wowote kuanzia sasa
ili wanaCCM wote wawe huru kumchagua kiongozi atakaye sukuma CCM UK toka hapa
tulipofikia.
Wakati huohuo Halmashauri Kuu
ya CCM ya Tawi la UK
jana iliazimia kwa pamoja kumsimamisha
Katibu wake wa Tawi Mariam Mungula baada ya majadiliano ya kina ya
kutokuridhishwa kabisa na utendaji na uratibu wake wa kazi.
Kikao hicho
kilipeleka shauri lake kwa Kamati ya Maadili na Usalama ili apate haki ya
kujitetea ni kwa nini asiachishwe moja kwa moja kazi yake za Ukatibu wa CCM UK. Ndugu Leybab Mdegela anakaimu nafasi yake
kuanzia jana 12/04/2014.
Kikao kiliendelea na hoja zake
za kuboresha Chama hapa UK
na kuweka mikakati yenye mawazo chanya katika kukisaidia chama katika mikakati
kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wote wa Tanzania.
Imetolewa
na
Abraham Sangiwa
Idara
ya Itikadi na Uenezi ya Halmashauri Kuu ya CCM UK.
13/04/2014.
Social Plugin