Forward this email [F]
Wakulima
kata ya Usanda wilaya ya Shinyanga wameiomba serikali kuchukuwa hatua
za haraka kuangamiza ndege waharibifu wa mazao kwelea kwelea ili
kunusuru mazao yao kumalizwa na kuwepo tishio la kukumbwa na njaa pamoja
na watoto kushindwa kuhudhuria masomo kwa kulinda ndege.
Wakiongea
na waandishi wa habari waliotembelea kata hiyo,walisema mazao yao
yanaliwa na ndege hao ukiwemo mpunga,mtama na uwele na kwamba wanahofia
kukosa chakula kutokana na kushambulia kwa kasi na kubakiza mabua pekee.
Mkulima
wa kijiji cha Manyanda Nyanda Jumanne alisema hali kwa sasa ni mbaya
na wanahitaji msaada wa haraka wa serikali, vinginevyo muda ukizidi
kwenda kabla ya
kuwadhibiti wakulima hawataambulia kitu na matokeo yake watakuwa
wamepoteza nguvu zao bure.
“ Makundi ya
ndege wa haribifu wanatua kila kukicha tunawaona tunajitahidi kukaa
mashambani kwa ajili ya kuwafukuza lakini wanatuzidi kwa kuwa ni
wengi,bora serikali ingetuma ndege ya kunyunyizia dawa ili kuwauwa bila
ya hivyo hakuna tunachokifanya”alisema Mussa.
Kwa upande wake
diwani wa kata hiyo Abeid Aljabiri,alisema ni maafa makubwa kutokana na
uharibifu unaofanywa na ndege hao na kuitaka serikali kusikia kilio cha
wakulima ,kupeleka ndege ya kunyunyizia dawa haraka kwa kuwa muda
unavyozidi kwenda ndivyo madhara yanatokea zaidi.
Alisema ndege
hao kwelea kwelea wanaharibu mazao ya mpunga ,mtama na
uwele wameharibu zaidi mazao katika kijiji cha
Shagaluba,Manyada,Nzagaluba,Singita na Igaganulwa na hali ni mbaya
katika vijiji hivyo ambapo wakati mwingine wazazi wamekuwa wakiwazuia
watoto kwenda shule ili walinde ndege.
Social Plugin