Maandamano ya kuelekea katika uwanja wa Taifa Mjini Kahama yaliojumuisha Timu 26 tayari kwa ufunguzi wa mashindano ya Mpesya Cup Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Ngaya FC katika uzinduzi wa mashindano ya Mpesya CUP yalionza juzi Wilayani Kahama Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akifungua mashindano ya Mpesya Cup yatakayosaidia kupata Timu ya Wilaya ya Kahama Baadhi ya Timu zilizoshiriki katika maandamano ya ufunguzi wa mashindano ya Mpesya CUP Wachezaji wa Timu mbalimbali wakiwa katika maandamno Wa kwanza kulia Mwenyekiti CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja ambaye pia alikuwa mmoja kati ya Viongozi walioshiriki katika maandamano hayo,wa kwanza kulia ni bwana Raymond Mihayo wa gazeti la Habari leo na mihayorj.blogspot.com
Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya Kahama Benson Mpesya na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja(wa kwanza kutoka kulia) wakiwa katika maandamano.
Serikali Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga imesema
kuwa haitawatupa Vijana hasa katika masuala mazima ya michezo kwa lengo la
kuinua uchumi wa Wilayani hiyo sambamba na kupata timu itakayoshiriki ligi kuu
kwa miaka ijayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyasema hayo
wakati akifungua mashindano ya Mpira wa miguu maarufu kama Mpesya cup ambayo
yanashirikisha jumla ya timu 26 za Wilaya ya Kahama.
Mpesya alisema kuwa haiwezekani Wilaya ya Kahama
pamoja na kuwa rasilimali nyingi ikiwemo wawekezaji katika sekta za migodi na
Tumbaku wapo lakini Wilaya inakosa timu inayoshiriki ligi kuu hapa nchini.
Alisema lengo la mashindano ya Mpesya cup
ni kukuza vipaji kwa Vijana wa Wilaya ya Kahama sambamba na kutafuta wachezaji
ambao wataunda timu ya kombaini ya Wilaya ya Kahama ambayo itashiriki katika
mashindano mbalimbali.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama alisema mpira ni starehe na unakuza akili na kuongeza kuwa hivi sasa pia ni ajira hali
ambayo itawafanya wachezaji kufanya michezo kama sehemu yao ya kujipatia
kipato.
“ Kwa sasa tumedhamiria ,Wilaya ya Kahama lazima tupate
timu itakayocheza ligi kuu ,Rasilimali tunazo,wachezaji
tumieni michezo katika kuonyesha vipaji vyenu ”,
Alisema Mpesya.
Pia aliwataka wachezaji kutumia michezo kama sehemu
ya kujenga urafiki na mahusiano mazuri
na kutoa onyo kwa waamuzi mashindano hayo kuhakikisha kuwa wanachezesha michezo
hiyo kwa kufuata sheria 17 za soka.
Katika michezo hiyo hiyo ya Mpesya cup mshindi wa
kwanza atapata zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na seti moja ya jezi,
kikombe na mpira mmoja wakati wa pili
atapa kiasi cha shilingi 500,000 pamoja na seti moja ya jezi na mpira .
Michuano hiyo tayari imeanza juzi kwa mechi moja
katika timu ya Ngaya FC na Ambassador na kumalizika kwa matokeo ya timu ya
Ambassador kuinfunga timu ya Ngaya FC kwa jumla ya mabao 2-1.
picha na stori kwa hisani ya mihayorj blog