Ni balaaa!!! PSPF WAKUTANA NA WAFANYABIASHARA MJINI SHINYANGA, WATOA ELIMU KUHUSU MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI,FUATILIA HAPA TUKIO ZIMA
Thursday, April 24, 2014
Ni
katika siku ya kwanza ya ziara ya afisa kutoka mfuko
wa pensheni wa PSPF (Public Service Pension Fund),Erick Chanimbaga,akiwa ameambatana na mjumbe wa bodi ya PSPF bwana Clement Mswanyama,mkoani Shinyanga iliyoanza leo
inayolenga kutembelea na kuhamasisha
wafanyakazi katika sekta binafsi wakiwemo wafanyabiashara,wafanyakazi wa
viwandani,waendesha bodaboda na wajasiriamali wa aina mbalimbali kwa ajili ya
kuwafahamisha,kuwahamasisha na kuwaelisha kuhusu mpango wa uchangiaji wa
hiari(pspf supplimentary scheme),mpango ambao umeanzishwa na PSPF kwa ajili ya
kupanua wigo wa uanachama kwa kuandikisha wananchi waliojiajiri au kuajiriwa
katika sekta rasmi na isiyo rasmi.Kulia ni Clement Mswanyama mjumbe wa bodi ya PSPF akizungumzia lengo la ziara yao,kushoto kwake ni afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga wakizungumza na wafanyabiashara katika soko kuu la mjini Shinyanga jioni ya leo
Kulia ni Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga akieleza kuhusu namna ya wanachama wa mpango wa uchangiaji hiari watakavyoweza kuwasilisha michango yao,ambapo alisema kuna namna tatu za kuchangia kama vile kwa wiki,mwezi au msimu kutegemea na upatikanaji wa kipato cha ziada kwa ajili ya akiba.Alisema michango hiyo itawasilishwa moja kwa moja kupitia akaunti ya benki au kwa wakala wa malipo wa M-PESA,TIGO PESA NA AIRTEL MONEY,ambapo kiwango cha uchangiaji ni kuanzia shilingi elfu kumi au zaidi.Alisema ofisi za PSPF katika mkoa wa Shinyanga zipo kwenye jengo la Benki ya posta ghorofa ya pili. Aidha Chanimbaga aliwaambia wafanyabiashara hao kuwa mara baada kujiunga na mfuko huo wanawezpa kupata taarifa zao njia tatu ambazo ni kwa kupiga simu namba 0225510400 ambayo ni kwa ajili ya huduma kwa wateja kwa njia ya simu, pia kwa kutumia huduma nyingine iitwayo pspf karibu nawe kwa kutuma ujumbe wa mfupi wa simu andika neno pspf kwenda namba 15357 au kwa kutembelea ofisi zozote za pspf,na kwa njia hizo anaweza kupata historia ya michango yake tangu mwanzo
Kushoto ni mwenyekiti wa soko kuu mjini Shinyanga bwana Alex Stephen,kulia kwake ni afisa masoko wa manispaa ya Shinyanga bwana Mabina Amani wakiwa ndani ya soko kuu wakifuatilia kilichokuwa kinazungumzwa na afisa pamoja na mjumbe wa bodi ya PSPF ambao walisema mfuko wa hifadhi ya jamii umepanuliwa ili watu kutoka katika sekta binafsi ili wanufaike na mfuko huo
Kulia ni mfanyabiashara katika soko kuu la mjini Shinyanga bwana Apolinari Mabula akifuatilia kwa umakini zaidi swali alilouliza kwa afisa kutoka PSPF mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa bodi ya PSPF kuhusu namna ya kuchangia na endapo kuna mafao yoyote kupitia mpango huo wa uchangiaji hiari
Kushoto ni bwana Clement Mswanyama mjumbe wa bodi ya PSPF akitaja aina ya mafao yaliyopo katika mpango wa uchangiaji wa hiari,ambapo alisema kuna mafao ya aina sita kama vile fao la Elimu,fao la ujasiriamali,fao la uzeeni,fao la kifo,fao la ugonjwa pamoja na fao la kujitoa.Mswanyama alisema ni wakati mzuri sasa kwa vijana kutumia fursa hiyo ya uchangiaji wa hiari kuweka akiba ya uzeeni ili wasipate taabu wakiwa wazee kwani fao hilo litalipwa kwa mwanachama aliyefikisha umri wa miaka 55 au zaidi ambapo mwanachama atalipwa akiba yake ya asilimia mia moja pamoja riba itakayokokotolewa.
Kulia ni bwana Clement Mswanyama mjumbe wa bodi ya PSPF kushoto kwake ni afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga wakinong'ona jambo ndani ya soko kuu la mjinin Shinyanga wakiwa katika ziara yao kuhamasisha wafanya kazi wa sekta binafsi kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari ulioanzishwa na PSPF kwa ajili ya kupanua wigo wa uanachama kwa kuandikisha wanachama wanaojiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi
Mbele ni Clement Mswanyama mjumbe wa bodi ya PSPF akizungumzia kuhusu fao la ujasiriamali ambapo alisema litatolewa kwa mwanachama ambaye amechangia kwenye mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi 12 ambapo nusu ya akiba ya mwanachama(50% ya michango) itatumika kulipa fao hilo na nusu itabaki katika akaunti ya mwanachama kwa ajili ya akiba ya uzeeni,na katika hili mwanachama atapaswa kuandika barua ya maombi
Mbele ni Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga,akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo ambapo alisema mpango wa uchangiaji wa hiari una umuhimu mkubwa kwa wafanyakazi kutoka sekta binafsi kwani uchangiaji wake unategemea na upatikanaji wa kipato cha ziada kwa ajili akiba na hakuna gharama ya kujiunga na mpango huo ila unatakiwa na picha moja ya pasipoti na hakuna ukomo wa uchangiaji
Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga akiwa ameambatana na mjumbe wa bodi ya PSPF kesho siku ya Ijumaa wataendelea na ziara yao mkoani Shinyanga ambapo wanatarajia kukutana na waendesha bodaboda,wafanyakazi wa viwandani na wajasiriamali pamoja na makundi ya aina mbalimbali mjini Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin