Idara ya
usafi wa mazingira wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imezifunga hoteli mbili
pamoja na nyumba tatu za kulala wageni
kutokana na kukosa miundo mbinu bora ya maji na vyoo
pamoja na mazingira machafu,ambapo hata mashuka katika sehemu hizo yameelezwa kuwa katika halim mbaya
Akizungumza
na waandishi wa habari wilayani Kishapu afisa mazingira wa wilaya hiyo Mohamed
Mlewa,amezitaja hoteli zilizofungwa kuwa ni Samaka hoteli,Kali na nyumba za
kulala wageni (gesti)tatu ambazo ni Uchunga gesti, Tulivu na Malaika na
imewataka wahusika kuboresha mapungufu yaliyojitokeza.
Amesema idara ya usafi wa
mazingira wilayani humo ilifanyanya ukaguzi na kubaini kuwa katika hoteli na nyumba hizo za
kulala wageni hazina huduma ya maji,kalo la maji machafu na miundombinu ya
ndani kutoridhisha,mashuka kuwa katika hali mbaya.
Mlewa amesema
hali ya mazingira kutoridhisha katika
sehemu hizo muhimu inahatarisha afya za
wateja kwani walibaini pia katika nyumba hizo za kulala wageni hata shuka
hazirdhishi hivyo wanafanya ukaguzi ili kuepuka milipuko ya magonjwa inayoweza
kutokea.
Amesema
walifanya zoezi hilo tarehe 27 mwezi Machi,mwaka huu katika mji wa Mhunze mji
mdogo wa Maganzo na kwamba wanaendelea
na zoezi hilo kwa wilaya nzima ili kuhakikisha mazingira yote yanakuwa safi.
Afisa
mazingira huyo amesema idara yake imeanza zoezi la kukagua hoteli ,nyumba za
kulala wageni na baa na kwamba hatua itakayofuata ni kukagua migahawa.
Social Plugin