Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Noma sanaaa!!! HOTELI NA GESTI ZAFUNGWA HUKO KISHAPU,MAZINGIRA MABOVU-,ZINGINE HAZINA MAJI,SHUKA ZAKUTWA KATIKA HALI MBAYA

Idara ya usafi wa mazingira wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imezifunga hoteli mbili pamoja na nyumba  tatu za kulala wageni kutokana na kukosa miundo mbinu bora ya maji na vyoo pamoja na mazingira machafu,ambapo hata mashuka katika sehemu hizo yameelezwa kuwa katika halim mbaya

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Kishapu afisa mazingira wa wilaya hiyo Mohamed Mlewa,amezitaja hoteli zilizofungwa kuwa ni Samaka hoteli,Kali na nyumba za kulala wageni (gesti)tatu ambazo ni Uchunga gesti, Tulivu na Malaika na imewataka wahusika kuboresha mapungufu yaliyojitokeza.
 
Amesema idara  ya usafi wa mazingira wilayani  humo ilifanyanya ukaguzi na kubaini kuwa katika hoteli na nyumba hizo za kulala wageni hazina huduma ya maji,kalo la maji machafu na miundombinu ya ndani kutoridhisha,mashuka kuwa katika hali mbaya.
 
Mlewa amesema  hali ya mazingira kutoridhisha katika sehemu hizo muhimu  inahatarisha afya za wateja kwani walibaini pia katika nyumba hizo za kulala wageni hata shuka hazirdhishi hivyo wanafanya ukaguzi ili kuepuka milipuko ya magonjwa inayoweza kutokea.
 
Amesema walifanya zoezi hilo tarehe 27 mwezi Machi,mwaka huu katika mji wa Mhunze mji mdogo wa Maganzo na kwamba  wanaendelea na zoezi hilo kwa wilaya nzima ili kuhakikisha mazingira yote yanakuwa safi.
 
Afisa mazingira huyo amesema idara yake imeanza zoezi la kukagua hoteli ,nyumba za kulala wageni na baa na kwamba hatua itakayofuata ni kukagua migahawa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com