Alhamisi ya wiki hii Kampuni ya magari ya Nissan imezindua gari jipya lenye uwezo wakipekee kabisa wa kujisafisha lenyewe na kuondoa kabisa uchafu wa aina yoyote ile kwenye gari hilo.
Watengenezaji hawa wa magari aina ya Nissan wamefanya majairibio kwenye gari hili kwa kutumia rangi maalum ya magari inayojulikama kwa jina la "Ultra-Ever Dry" ambayo ina ondoa uchafu kwenye gari na kufanya gari kujisafisha lenyewe.
Aina hii ya rangi ni maalum kwa kuzuia maji na mafuta kupenyeza au kuganda juu ya rangi hii.
Kampuni ya nissan wametoa taarifa rasmi na kusema kuwa ....
"Kwa kujenga tabaka la kinga ya hewa kati ya rangi na mazingira, kwa ufanisi kabisa inazuia maji na uchafu wa barabara, kuunda na kuacha alama chafu juu ya rangi ya gari, " Nissan walisema katika taarifa yao
Nissan wamesema kuwa Rangi hii inayo zuia uchafu kwenye gari, kwa hivi sasa imefanyiwa majaribio kwenye gari aina yaNissan Note na imeonyesha mafanikio mazuri kabisa katika mazingira yote ikiwa ni katika sehemu zenye hali ya hewa ya kawaida, sehemu zenye barafu, pamoja na sehemu zenye maji maji.
Nissan wameendelea kusema kuwa bado mafundi wao wanaendelea kufanya majaribio ya rangi hii kwenye kituo chao cha ufundi huko ulaya.
TAZAMA VIDEO YAKE HAPA