Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PICHA-HUYU NDIYO MTANGAZAJI WA NOOR FM YA ZANZIBAR ALIYEJIRUSHA GHOROFANI WAKATI REDIO HIYO IKITEKETEA MOTO


DSC_1964
Aboubakar Fakih Mtangazaji wa Radio Noor FM 93.3 na ni muajiriwa wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Pichani akiwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu ambapo amepata Ajali na kukatika mguu mmoja na mwengine kuumia pamoja na mkono ajali iliyosababishwa na hitilafu ya umeme katika Studio  Masjid Swahaba Mtoni Zanzibar, aliumia baada ya kujirusha kutoka Juu ya Ghorofa Moja.
DSC_1965
Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim. Seif Sharif Hamad akisalimiana na Aboubakar Fakih Mtangazaji wa Radio Noor FM 93.3 na muajiriwa wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar alipokwenda kumtembelea Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
DSC_1968
Dokta wa Mifupa Said Omar (Gaza) akiwaonyesha Maalim Seif Sharif Hamad na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abdallah Mwinyi Khamis sehemu aliyokatika Aboubakar Fakih,  walipoenda kumjulia hali.
DSC_1984
 Wakimuombe Duwa.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com