Waangalizi
katika Uchaguzi wa Ubunge Chalinze wamesema Jeshi la Polisi lilielekeza
ulinzi kwenye mikutano ya CCM zaidi na kuviacha vyama vingine vikiwa
havina ulinzi.
Waangalizi hao ni Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Mashirika ya Haki za Binadamu Kusini mwa
Afrika (Sahringon) walisema vyama vya Chadema, CUF, NRA na AFP
havikupewa na ulinzi.
Akizungumza jana, Mratibu wa Taifa wa Sahringon,
Martina Kabisama alisema ulinzi wa polisi ulikuwa kwenye mikutano ya CCM
na si kwa vyama vingine hali ambayo ingeweza kuathiri usalama wa maeneo
hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei
hakupatikana jana kuzungumzia madai hayo, lakini msaidizi wake, Steven
Kiango alisema bosi wake atalitolea ufafanuzi suala hilo, Jumatatu. “Kwa
sasa Kamanda Matei yuko nje ya ofisi na siwezi kulizungumzia hilo,
nitamfahamisha na atalitolea ufafanuzi Jumatatu,” alisema Kiango.
Kabisama alisema: “Kwa mfano, siku ya kufunga
kampeni timu ya uangalizi ilishuhudia ulinzi mkubwa kwenye mikutano ya
CCM lakini Chadema na CUF hakukuwa na askari hata mmoja,” alisema.
Alisema waangalizi hao pia walibaini lugha za
maudhi, kashfa na kejeli katika kampeni za vyama vya CCM, Chadema na
CUF.
“Tunapendekeza Msajili wa Vyama vya Siasa atoe karipio kali kwa vyama hivyo kuhusu matumizi ya lugha za vitisho, kashfa na kejeli,” alisema.
“Tunapendekeza Msajili wa Vyama vya Siasa atoe karipio kali kwa vyama hivyo kuhusu matumizi ya lugha za vitisho, kashfa na kejeli,” alisema.
Alipendekeza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec),
kuifanyia marekebisho Sheria ya Uchaguzi ili kuwazuia viongozi wakuu wa
serikali kushiriki kwenye kampeni.
Na Raymond Kaminyoge na Sanjito Msafiri
Na Raymond Kaminyoge na Sanjito Msafiri
Social Plugin