Ridhiwani Kikwete aliyekuwa mgombea ubunge uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze Bagamoyo
mkoani Pwani kupitia chama cha mapinduzi CCM, ameibuka
kidedea kwa asilimia 86.61 katika uchaguzi huo na kuwamwaga wagombea
wengine kutoka vyama vinne vya upinzani.
Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha Ridhiwani ameongoza akifuatiwa na CHADEMA ,CUF,NRA na ASP.
Matokeo hayo yametangazwa usiku wa kuamkia leo April 7 majira ya saa
nane usiku katika shule ya sekondari Chalinze na Msimamizi wa uchaguzi
huo Bw.Samwel Salianga ambapo amesema CCM – Ridhiwani Kikwete amepata kura 20,828 sawa na
86.61%, Chadema -Mathayo Torongei amepata kura 2,544 sawa na asilimia
10.58,CUF- Fabian Skauki 476 sawa na asilimia 1.98,NRA Hussein
Ramadhani kura 60 asilimia 0.25 huku AFP Ramadhani Mgaya amepata
kura 186 sawa na asilimia 0.59.
Salianga amesema kati ya watu waliojiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura ni watu elfu 92,waliojitokeza
katika zoezi hilo ni watu 24,422 ambapo kura halali zilikuwa 24,047 na
kura 375 zikiharibika.
Wagombea waliokuwepo wakati wa kutangaza matokeo katika uchaguzi huo na kusaini fomu ya kukubalina na matokea alikuwepo mgombea wa NRA na CCM pekee.
Aidha Wakizungumza baada ya kupokea matokeo hayo aliyekuwa mgombea wa
chama cha NRA pamoja na Ridhiwani Kikwete kupitia CCM,kila Mmoja
ameshukuru wananchi na kuahidi kushirikina na wananchalinze kuleta
maendeleo.