Shinyanga Leo- MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WAKUTANA NA WADAU WAKE SHINYANGA,WAPATA CHAKULA PAMOJA NA KUBADILISHANA MAWAZO
Saturday, April 26, 2014
Wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Anna rose Nyamubi,akifuatiwa katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselim Tarimo aliyekuwa mgeni rasmi,na Aliyesimama ni Mjumbe wa bodi ya mfuko wa pensheni wa PSPF (Public Service Pension Fund) Clement Mswanyama akizungumza jana usiku wakati kikao cha majumuisho ya ziara ya PSPF ya siku 2 mkoani Shinyanga pamoja na kupata chakula cha pamoja na wadau mbalimbali wa mfuko huo katika ukumbi wa Vigimark Hotel mjini Shinyanga akitoa hotuba fupi. Pamoja na mambo mengine alisema lengo la ziara yao iliyoanza Tarehe 24 April hadi 25,mwaka 2014 ililenga kukutana na wadau wa PSPF,hususani kutoka sekta binafsi na kuwapa elimu kuhusu mpango wa uchangiaji wa hiari (PSPF Supplimentary Scheme) ambao utawanufaisha watu wote mfano walioajiriwa au waliojiajiri kwani wataweza kuchangia kidogo kidogo kuanzia shilingi 10,000/= na hakuna kima cha juu
Awali Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa
Shinyanga Erick Chanimbaga akizungumza katika ukumbi wa Vigimark Hotel jana usiku,ambapo alisema katika ziara yao ya siku 2,wameweza kukutana na wakulima,wafanyabiashara,wafanyakazi wa viwandani,waendesha bodaboda,madereva taxi pamoja na makundi mbalimbali ya wajasiriamali na kuwapa elimu kuhusu mfuko wa PSPF unaomwezesha mwanachama kuchangia kwa hiari
Aliyesimama ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselim Tarimo akizungumza katika hafla hiyo fupi ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kujiunga na mfuko hifadhi wa PSPF ili kujiwekea akiba ya uzeeni na kutolea mfano kuwa wazee waliowengi wanaohangaika hivi sasa mfano kuomba omba wangekuwa wamejiwekea akiba mapema wasingefikia hatua hiyo
Wadau mbalimbali wakiwa ndani ya ukumbi wa Vigimark Hotel ambako mgeni rasmi alikuwa katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Anselim Tarimo wakati wa kikao cha majumuisho na chakula cha pamoja kilichoandaliwa na PSPF taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoanzishwa na sheria ya mafao hitimisho la kazi kwa watumishi wa umma namba 2 ya 1999 sura ya 371.
Kikao cha majumuisho kinaendelea -PSPF inatoa huduma za kijamii kwa mfumo wa hiari na ule wa lazima,ambapo hivi sasa mfuko wa PSPF unahudumia wanachama na wategemezi zaidi ya 400,000 kutoka sekta mbalimbali.
Akizungumza katika ukumbi huo afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga alieleza kuwa ofisi za PSPF katika mkoa wa Shinyanga zipo katika jengo la Galame Traders( jengo la benki ya posta mjini Shinyanga ghorofa ya pili
Katika mpango wa uchangiaji wa hiari kuna mafao ya aina sita kama vile
fao la Elimu,fao la ujasiriamali,fao la uzeeni,fao la kifo,fao la ugonjwa
pamoja na fao la kujitoa
Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa
Shinyanga Erick Chanimbaga akiwashukuru wadau wa PSPF waliofika katika hafla hiyo fupi na kuwaomba wajiunge na mfuko huo wa uchangiaji wa hiari kwani una faida kwa aliyejiajiri mwenyewe na hata aliyeajiriwa
Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga aliwaambia wadau hao wa PSPF kuwa uchangiaji katika mpango wa uchangiaji wa hiari unategemea na
upatikanaji wa kipato cha ziada kwa ajili akiba na hakuna gharama ya kujiunga
na mpango huo ila unatakiwa na picha moja ya pasipoti na hakuna ukomo wa
uchangiaji
Wadau wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo fupi walipata muda wa kula na kunywa vinywaji vya kila aina kama unavyoona pichani .
Social Plugin