Mwimbaji Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma, Muhidin Maalim Gurumo amefariki dunia mchana wa leo.Ni
mzee wa siku nyingi sana kwenye muziki Tanzania,amekuwa kwenye bendi hiyo zaidi ya miaka 50,ni mzee ambae aliwahi kuingia
kwenye vichwa vya habari mara nyingi hasa kutokana na kuugua kwake
kuliko mfanya aache hata muziki aliokua anaufanya.
Taarifa zilizothibitishwa na hospitali ya Taifa Muhimbili zimesema Mzee huyu amefariki dunia akiwa hospitalini hapo leo April 13 2014 saa nane mchana baada ya kuletwa jana asubuhi na kulazwa kwenye wodi namba 6 ya Mwaisela kutokana na kuzidiwa.
Imeelezwa kuwa mzee Gurumo amefariki kutokana na maradhi ya moyo.
Tayari mwili wake umepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba msiba uko nyumbani kwake Mabibo Makuburi.
Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Gurumo.Amina!!
Tayari mwili wake umepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba msiba uko nyumbani kwake Mabibo Makuburi.
Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Gurumo.Amina!!
Social Plugin