Tabora kwanuka Damu_MAJAMBAZI YAUA ASKARI POLISI WAWILI KWA RISASI,TAZAMA PICHA HAPA
Tuesday, April 29, 2014
Baadhi ya askari Polisi wakiutoa mwili wa askari Polisi kwenye Wodi namba moja aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi huko katika Tarafa ya Ussoke wilayani Urambo askari huyo aliyefahamika kwa namba F.5179 PC JUMANNE,walipigwa risasi wakiwa na askari mwenzake ambaye pia alifariki papo hapo namba G.3388 PC SHABAN.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP SUZAN KAGANDA akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la mauaji ya askari Polisi wawili ambao waliuawa wakati wakijitayarisha kukabiliana na Majambazi watatu waliovamia nyumbani kwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la IBRAHIMU MOHAMED mkazi wa Ussoke ambapo walipora zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili pamoja na vocha za simu zenye thamani ya shilingi laki moja na ishirini elfu.Kamanda SUZAN alisema majambazi hayo yalikuwa yakitumia bunduki aina ya SMG.
Mwili wa askari namba F.5179 PC JUMANNE ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete,askari huyo alifariki dunia wakati madaktari wakijaribu kuokoa uhai wake kufuatia kujeruhiwa kwa kupigwa risasi tumboni na majambazi matatu huko Ussoke wakati askari huyo akiwa anajipanga na mwenzake kukabiliana na majambazi hayo yaliyovamia nyumbani kwa mfanyabiashara mmoja Ibrahimu Mohammed.
via>>Kapipij blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin