Afisa uhusiano na wateja TANESCO Mkoa wa Shinyanga bwana Amoni Michael akizungumza wakati wa kikao cha makamanda wa jeshi la jadi sungusungu |
Shirika la
umeme nchini TANESCO mkoa wa Shinyanga limeliomba Jeshi la jadi sungungu na
wakazi wote wa mkoa huo kushirikiana na
shirika hilo katika kulinda miundo mbinu ya shirika hilo kwa kuwafichua watu wote wanaohujumu miundombinu
hiyo kama vile kuiba nyaya,mita,mafuta ya transfoma.
Wito huo umetolewa
jana na afisa uhusiano na wateja TANESCO Mkoa wa Shinyanga bwana Amoni Michael
wakati wa kikao cha makamanda wa jeshi la jadi sungusungu maarufu kwa jina la
Sanjo kutoka katika wilaya ya Shinyanga vijijini,Shinyanga mjini na wilaya ya
Kishapu kilichofanyika katika shule ya Msingi Kolandoto kata ya Kolandoto
katika manispaa ya Shinyanga.
Afisa huyo
wa TANESCO aliwataka Sungusungu kusaidiana na shirika hilo pamoja wananchi kuwabaini
wanaohujumu miundo mbinu kama vile mita,transimita,nguzo na nyaya kwani
panapotokea uhujumu kuna athari kubwa kiuchumi na kijamii kwani asilimia kubwa
vitu vingi vinatumia umeme hivyo kama hakuna umeme hata ghrama za maisha
zinapanda.
Alisema ni
vyema wananchi wakashiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme huku
akiwatahadharisha wanaolima katika eneo la njia ya umeme kuacha kufanya
shughuli za kiuchumi kwani wanaweza kupata matatizo ikiwemo kupoteza maisha
kutokana na wananchi wasio waaminifu kuharibu miundombinu ya umeme.
Naye
mhandisi wa njia kuu za umeme mkoa wa Shinyanga Job Bidya alisema serikali na TANESCO
zinapata hasara kubwa pindi miundombinu inapohujumiwa hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za
shirika hilo katika kuzalisha,kusafirisha na kusamabaza umeme kwa wateja wake.
Bidya alisema TANESCO itatoa zawadi kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi kuhusu
wanaohujumu miundombinu.
Nao viongozi
wa sungungu walisema watatoa ushirikiano kwa mamlaka mbalimbali kama vile za umeme,maji,reli,barabara na simu katika
kulinda miundo mbinu yao kwani hasara zinazotokana na kuharibu miundombinu hiyo zinawaathiri wananchi wote ndiyo maana wakaamua kuitisha
kikao na mamlaka hizo ili kuangalia namna ya kupambana na wanaohujumu
miundombinu hiyo.
Social Plugin