WACHEZAJI WALIOONGEZWA KWENYE KIKOSI CHA TAIFA STARS,WATAKAOINGIA KAMBINI KESHO

kilimanjaro_stars__
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga ametangaza
wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho Aprili 20 kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi ambayo itachezwa Aprili 26 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam),Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadili Ali (Azam) upande wa mabeki ni Abdi Banda (Coastal Union),Aidan Michael (Ruvu Shooting),Aggrey Morris (Azam),Erasto Nyoni (Azam),Hassan Mwasapili (Mbeya City),Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam).
Upande wa Viungo ni Amri Kiemba (Simba),Frank Domayo (Yanga),Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba)na Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).
Washambuliaji niMohammed Seif Saidi (Kusini Pemba),Ayoub Kasim Lipati (Ilala),Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi),Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 niMbwana Mshindo Musa (Tanga) naBayaga Athanas Fabian (Mbeya).
Taifa Stars inategemewa kuingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.
Via>>TZA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post