Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Ukatili!! NJEMBA YABAKA MTOTO WA MIAKA 4



 
Jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Iddi Mgosi anashikiliwa na Polisi wa Kituo cha Wazo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minne (jina linahifadhiwa) huko Mivumoni, Madale Machi 18, mwaka huu.

Mgosi, ambaye umri wake haukuweza kupatikana mara moja, anadaiwa kumrubuni mtoto huyo kutoka nyumbani kwao na kumpeleka kwake, ambako alimuingilia kwa nguvu na baadaye kumtisha kutosema lolote kwa wazazi wake.

Mama mzazi wa mtoto huyo, aligundua mwanaye kuwa na maumivu makali wakati akimuogesha, kwani alipomshika sehemu zake za siri, binti huyo alipiga kelele za maumivu na alipoulizwa kilichomsibu ndipo alipoelezea alichofanyiwa.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, mama huyo aitwaye Hadija, alisema alikuwa akimuogesha mtoto wake huyo bila kugundua kwamba alikuwa amebakwa na kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri. Alipomshika kwa ajili ya kumsafisha, mtoto huyo akaanza kulia na kulalamika kwamba alikuwa akimuumiza.

Bi Hadija alisema mara baada ya kuambiwa hivyo, akawaita ndugu zake na kuwasimulia alichoambiwa hivyo wote kwa pamoja wakachukua jukumu la kumfuata Mgosi, kumkamata na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Wazo.

Baada ya kumuogesha binti yake, wakampeleka katika hospitali ya Mwananyamala alikochukuliwa vipimo kadhaa na kuambiwa wampeleke mtoto huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Hospitalini walituambia kwamba sehemu zake za siri zimeharibiwa sana na hata kibofu chake cha mkojo pia kimeharibiwa kwani wametoa uchafu mwingi. Kwa sasa amelazwa hospitalini huku akiendelea kupatiwa matibabu na hawajajua ni siku gani ataruhusiwa.”

Waandishi wetu hawakuishia hapo, walimfuata mtoto na kumuuliza maswali kadhaa kwa lengo la kujiridhisha ambapo alisema:

“Mgosi alinichukua, akaniambia twende kwake, tulipofika huko akanivua nguo na kunilalia...ameniumiza,” alisema mtoto huyo huku akionekana bado kuwa kwenye maumivu makali.
 
Baada ya kumpeleka Mgosi katika kituo cha Wazo, aliwekwa rumande na kufunguliwa jalada la mashtaka WH/RB/1891/2014KUBAKA.

Na Haruni Sanchawa/Nyemo Chilongani

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com