UNAFIKIRI NANI ATAWATETEA HAWA?? WANANYANYASIKA KILA KUKICHA
Saturday, April 19, 2014
Bado maeneo ya mikoa ya Shinynga na Simiyu imeonekana
kuwa wakazi wake wana tabia ya kuwanyanyasa wanyama kama inavyojieleza katika
picha ambapo kamera za mtandao huu wa malunde1 blog ziliwanasa wanyama hawa aina
ya punda wakiwa wamebebeshwa mizigo mizito zikiwemo injini za gari,matairi na
vyuma mbalimbali kinyume na taratibu za haki za wanyama katika kijiji cha
Wigelekelo wilaya ya Maswa mkoa mpya wa Simiyu.
Wanyama wameendelea kunyanyaswa wakati asasi nyingi za kutetea haki za wanyama kama vile Tanzania Animals Pritection Organisation (TAPO)yenye makao yake jijini Dar es salaam na ofisi yake iliyopo Kahama mkoani Shinyanga na wahusika wengine wengi wakiwa wamekaa kimya. Ng'ombe,mbwa,punda,paka na hata ndege wafugwao wamekuwa wakinyanyasika kwa kupigwa,kutopata huduma za afya,kubebeshwa mizigo mizito,kutopewa chakula. Je ni nani atakayewatetea wanyama hawa!??
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin