Wakazi wawili wa kijiji cha Mazombe,
mkoani Iringa wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za
kukutwa na kidole cha binadamu kwa kile kinachodaiwa kuwa kutokana na imani za kishirikina.
Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi
Mkoani Iringa, Wankyo Nyigesa alisema tukio hilo limetokea juzi na kuwataja watuhumiwa
hao kuwa ni Gibson Kasenegala (29) na Benson Mlasu (23).
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walikuwa wakimiliki kidole hicho ambacho hakijulikani kuwa ni cha nani,
ambapo inasemekana kwamba wakiwa na kidole hicho kinaweza kuwasaidia kupata mali.
“Tumewatia mbaroni na uchunguzi
wetu unaendelea ili tujue nani alikatwa kidole, au kama
kuna mtu aliuawa kisha kidole chake kikachukuliwa,” alisema Nyigesa.
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi huo kukamilika.
Na Frank Kibiki-Iringa
Social Plugin