Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UTAFITI WAONESHA KUNA WANAFUNZI WA VYUO WANAFANYA NGONO KWA BEI CHEE NA WENGINE BEI YA JUU HUKO IRINGA


Utafiti uliofanywa na mtandao wa tuko wangapi, Tulizana  mkoani Iringa, umebaini kuwepo kwa mtandao mkubwa wa ngono kwenye vyuo vikuu huku baadhi ya wasichana wa vyuo hivyo wakiamua kufanya biashara ya ngono wa lengo la kutafuta fedha za kujikimu kimaisha.
 
Utafiti huo unaonyesha kuwa, baadhi ya wanafunzi wa kike wanaosoma katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Ipogolo mjini Iringa, wanapendwa na wanaume wengi kwa madai ya kufanya biashara ya ngono kwa bei nafuu (chee) huku wale wa Chuo kikuu cha Iringa, zamani Tumaini wakisifika kuwa na gharama kubwa, kutokana na usomi wao.
 
Akitoa mada kwa waandishi wa habari wakati wa maandalizi ya kampeni ya kupunguza mtandao wa ngono kwenye vyuo vikuu vya Iringa, Mmoja wa maafisa wa kampeni hiyo,  Abou Msemo alisema hali hiyo imewasukuma kutoa mafunzo kwa wanafunzi hao ili kuwasaidia wajitambue.
 
Alisema ukweli ni kwamba, asilimia 80 ya maambukizi ya Ukimwi, inatokana na kuwepo kwa mtandao mkubwa wa ngono jambo ambalo ni hatari.
 
“Baada ya utafiti wetu tumebaini kuwa ukitaka mwanamke msomi kwa bei chee basi utampata chuo cha maendeleo ya jamiii cha Ipogoro lakini ukitaka wa gharama, huna budi kumfuata Tumaini-Iringa, hii ni hatari kubwa,”anasema Msemo.
 
Alisema baadhi ya mabinti waliohojiwa walisema wanalazimika kuingia kwenye mtandao wa ngono kutokana na ugumu wa maisha, japo elimu ya ukimwi imeshawafikia.
 
Kutokana na hali hiyo, tume ya kudhibiti ukimwi nchini TACAIDS na wizara ya afya wameamua kutoa elimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu mkoani Iringa kupitia tamasha la tuko wangapi, litakalofanyika keshokutwa katika uwanja wa Samora...Iringa mjini
 NA Tumaini Msowoya, Iringa
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com