Utafiti uliofanywa na mtandao wa
tuko wangapi, Tulizana mkoani Iringa,
umebaini kuwepo kwa mtandao mkubwa wa ngono kwenye vyuo vikuu huku
baadhi ya wasichana wa vyuo hivyo wakiamua kufanya biashara ya ngono wa
lengo la kutafuta fedha za kujikimu kimaisha.
Utafiti huo unaonyesha kuwa, baadhi ya
wanafunzi wa kike wanaosoma katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Ipogolo
mjini Iringa, wanapendwa na wanaume wengi kwa madai ya kufanya biashara ya ngono
kwa bei nafuu (chee) huku wale wa Chuo kikuu cha Iringa, zamani Tumaini wakisifika kuwa
na gharama kubwa, kutokana na usomi wao.
Akitoa mada kwa waandishi wa
habari wakati wa maandalizi ya kampeni ya kupunguza mtandao wa ngono kwenye
vyuo vikuu vya Iringa, Mmoja wa maafisa wa kampeni hiyo, Abou Msemo alisema hali hiyo imewasukuma kutoa
mafunzo kwa wanafunzi hao ili kuwasaidia wajitambue.
Alisema ukweli ni kwamba,
asilimia 80 ya maambukizi ya Ukimwi, inatokana na kuwepo kwa mtandao mkubwa wa
ngono jambo ambalo ni hatari.
“Baada ya utafiti wetu tumebaini
kuwa ukitaka mwanamke msomi kwa bei chee basi utampata chuo cha maendeleo ya
jamiii cha Ipogoro lakini ukitaka wa gharama, huna budi kumfuata
Tumaini-Iringa, hii ni hatari kubwa,”anasema Msemo.
Alisema baadhi ya mabinti
waliohojiwa walisema wanalazimika kuingia kwenye mtandao wa ngono kutokana na
ugumu wa maisha, japo elimu ya ukimwi imeshawafikia.
Kutokana na hali
hiyo, tume ya kudhibiti ukimwi nchini TACAIDS na wizara ya afya wameamua
kutoa elimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu mkoani Iringa kupitia tamasha
la tuko wangapi, litakalofanyika keshokutwa katika uwanja wa
Samora...Iringa mjini
NA Tumaini Msowoya, Iringa