Baraza la umoja wa vijana wa chama cha
mapinduzi [uvccm] wilaya ya Sengerema mkoa Mwanza limemvua madaraka
mwenyekiti wa umoja huo wilayani humo Robert Madaha ambaye pia alikuwa ni
diwani wa kata ya chifunfu kupitia(CCM) baada ya kuuza mali za
umoja huo
Ufagio huo pia umempitia katibu wa umoja wa vijana Benedict Bujiku ambaye naye
amevuliwa wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuuza mali za umoja huo bila lidhaa
ya baraza hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,
katibu wa chama cha mapinduzi [ccm] wilaya sengerema Mohamed shabani Mohamedi amesema
baraza hilo limefikia uamuzi huo kutokana na viongozi hao kuuza mali za jumuiya
hiyo kinyume na utaratibu na kutokushirikisha baraza hilo.
Amezitaja mali hizo kuwa ni pikipiki tano , gunia mbili za mpunga pamoja
na kibali cha kuvuna miti kilichotolewa na wizara ya maliasili na utalii kwa
jumuia hiyo kwa lengo la kupata mtaji wa kujiendesha.
Bw, Mohamed alisema kuwa baada ya kubaini
hayo baraza hilo liliitisha kikao cha dharura kilichokaa april 13 mwaka huu na
kuamua kuwavua madaraka hayo pia kuwa amuru kurudisha mali hizo za umoja huo .
Aidha amefafanua kuwa vikao mbalimbali vya
chama hicho vitakaa na kutoa mapendekezo kwa lengo la kuwavua uanachama kwa
kuwa wanakiabisha chama kutokana nyadhifa zao walizokuwa nazo kufanya mambo ya
kipuuzi yasiyo na maana ya kuhujumu mali za jumuia hiyo.