Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UVCCM WATIBUANA HUKO SENGEREMA,MWENYEKITI NA KATIBU WAKE WAVULIWA NYADHIFA ZAO


 

Baraza la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi [uvccm] wilaya ya Sengerema mkoa Mwanza limemvua  madaraka mwenyekiti wa umoja huo wilayani humo Robert Madaha ambaye pia alikuwa ni diwani wa kata ya chifunfu kupitia(CCM) baada ya kuuza mali za umoja huo

Ufagio huo pia umempitia katibu wa umoja wa vijana Benedict Bujiku ambaye naye amevuliwa wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuuza mali za umoja huo bila  lidhaa ya baraza hilo.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, katibu wa chama cha mapinduzi [ccm] wilaya sengerema Mohamed shabani Mohamedi amesema baraza hilo limefikia uamuzi huo kutokana na viongozi hao kuuza mali za jumuiya hiyo kinyume na utaratibu na kutokushirikisha baraza hilo.

Amezitaja mali hizo kuwa ni pikipiki tano , gunia mbili za mpunga  pamoja na kibali cha kuvuna miti kilichotolewa na wizara ya maliasili na utalii kwa jumuia hiyo kwa lengo la kupata mtaji wa kujiendesha.


Bw, Mohamed alisema kuwa baada ya kubaini hayo baraza hilo liliitisha kikao cha dharura kilichokaa april 13 mwaka huu na kuamua kuwavua madaraka hayo pia kuwa amuru kurudisha mali hizo za umoja huo .

Aidha amefafanua kuwa vikao mbalimbali vya chama hicho vitakaa na kutoa mapendekezo kwa lengo la kuwavua uanachama kwa kuwa wanakiabisha chama kutokana nyadhifa zao walizokuwa nazo kufanya mambo ya kipuuzi yasiyo na maana ya kuhujumu mali za jumuia hiyo.


 Na Valence Robert-Sengerema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com