Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UVCCM WATUA SHINYANGA NA PIKIPIKI ZAO,WAPIGIA DEBE SERIKALI MBILI


Viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mkuu wa wilaya ya Shinyanga pamoja na viongozi wa ccm mkoa wakiwa eneo la jukwaa kuu katika viwanja vya Shy-com mjini Shinyanga,wakisaini kitabu cha wageni


Kiongozi  wa matembezi hayo taifa anayetoka kanda ya Ziwa Zuberi Bundala akizungumza katika viwanja vya Shy-com ambapo alisema wameamua kuzunguka wilaya zote za kanda ya Ziwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu muungano na kuongeza kuwa vijana wa CCM wanataka serikali mbili ambazo wananchi wanalipa kodi na kuona matokeo ya kodi zao.


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akizungumza katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Shy-com mjini Shinyanga wakati wa matembezi ya mbio za pikipiki ambapo pamoja na kupigia debe serikali mbili pia alieleza kushangazwa na baadhi ya watu wanaotaka hati ya muungano na kuwafananisha na mtoto anapozaliwa na akikua aanze kudai na kulilia hati ya  ndoa ya baba na mama yake mzazi na kuwataka kuacha kubeza muungano.

Matembezi ya mbio za pikipiki taifa za kuenzi muungano wa Tanzania Zuberi yayoandaliwa na  umoja wa vijana  wa chama cha Mapinduzi (UVCCM)  taifa,yamebeba ujumbe wa  dumisha  muungano  vijana  kwa fursa  zilizopo kwa maendeleo yetu.
Uzinduzi wa mbio hizo za pikipiki ulifanyika mkoani Mara alikozaliwa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere na ambapo vijana wa ccm walidai  njia bora ya kumuenzi ni kutetea serikali mbili badala ya kufanya unafiki wa kutaka serikali tatu.
Matembezi ya mbio za pikipiki kuenzi muungano wa miaka 50 wa  Tanzania bara  na  Zanzibar  ulizinduliwa rasmi tarehe 22 machi mwaka huu   na  rais wa Zanzibar  Dkt  Mohamed Shein na kwa upande  kanda ya ziwa yalianza  rasmi tarehe 11 mwezi  huu .

 
 Matembezi ya mbio za pikipiki ya vijana wa CCM yakiendelea

Awali Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Simiyu Njau akikabidhi waendesha pikipiki kwa uongozi wa CCM mkoa wa Shinyanga katika kijiji cha Wigelekelo wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com