Vijana waliomaliza elimu ya sekondari na kushindwa
kuendelea na masomo ya elimu ya ngazi ya juu katika
manispaa ya shinyanga wameshauriwa kujiunga na
vyuo mbalimbali hapa nchini ili kujenga taifa la watu wasomi badala ya kukaa vijiweni
Hayo yamezungumzwa jana na mratibu wa kongamano la Elimu ya Ushauri Walter Lema kutoka chuo cha usimamizi wa Fedha cha Luther kilichpo
jijini Mwanza, wakati akitoa elimu ya ushauri kwa vijana waliomaliza elimu ya
kidato cha Nne na kuendelea mjini
Shinyanga ambao hawana taaluma yeyote na kuamua kukaa nyumbani bila kazi.
Elimu hiyo imetolewa katika viwanja vya Mazingira senta Mjini Shinyanga kwa lengo la kuwasaidia vijana waliokata tamaa na maisha kubadilika na kuzitumia fursa zinazopatika na hapa nchini.
Alisema vijana wengi hapa nchini wamekuwa wakikata tamaa na maisha pale wanaposhindwa kujiunga na elimu ya juu na
kuamua kukaa nyumbani bila kazi hali ambayo inachangia kuongezeka kwa idadi
kubwa ya vijana kutokuwa na ajira
Naye mwezeshaji
wa pili wa elimu hiyo bi Upendo Dickson aliwataka vijana hao pale wanapotaka
kujiunga na vyuo hivyo vya Taaluma wachague fani ambazo zitawapatia fursa ya
kupata ajira kwa urahisi ikiwani pamoja na kuchagua fani ambayo wanaipenda na
sio kushinikizwa
Bi Dickson alisema hivi sasa hapa nchi kuna fursa nyingi ambazo zinapatikana tofauti na
kipindi cha nyuma, hivyo vijana na wanatakiwa kuzitumia fursa hizo kwa
kujipatia kipato na kuinua uchumi wa Taifa kuliko kukaa nyumbani bila kazi huku
akisema kuwa kufeli mtihani sio kufeli maisha
Social Plugin