Klabu
ya Manchester United leo mchana imesafiri kuelekea jijini Munich kwa
ajili ya kupambana na Bayern Munich katika mchezo wa pili wa hatua ya 16
bora.Katika listi ya wachezaji waliosafiri na timu hiyo jina la
mshambuliaji Wayne Rooney lilikuwepo pamoja kwamba iliripotiwa anaweza
asiichezee timu hiyo kesho, lakini majina ya kiungo Marouane Fellaini na
mlinzi Rafael hayakuwemo katika listi ya wachezaji waliosafiri na timu
kwenda Munich ikielezwa kwamba wana majeruhi na hivyo hawataichezea timu
hiyo.
United tayari imewasili Ujerumani na leo jioni walifanya mazoezi katika uwanja wa Allianz Arena kujiandaa na kipute cha kesho.
Timu hizo zilitoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Old Trafford wiki iliyopita.
Social Plugin