Wizara ya Fedha kupitia Naibu wake Waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba wametangaza uamuzi wa kufuta malipo ya Wabunge waliosusia vikao vya mchakato wa Katiba vinavyoendelea Dodoma.
Uamuzi huu umetangazwa ikiwa ni siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka matusi na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu April 10 20014 baada ya Waziri wa Fedha kupata safari ya kikazi nchini Marekani,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato huo wa Katiba.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza Benki zote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance ambazo zilipelekwa Bungeni April 16 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka April 30.