Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BABA AUA KIJANA WAKE WA MIAKA 6 KWA KUMNYONGA KISHA KUMZIKA SHAMBANI



JESHI la Polisi Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma linamshikilia Mkazi wa Kijiji cha Likweso kilichopo katika kata ya Mchoteka aliyefahamika kwa jina la Mitaho Rashid Katona kwa tuhuma za kumuua kwa kumnyonga Mtoto wake wa Miaka 6 na kumzika shambani kwake.

Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa pamoja na mtuhumiwa huyo kutekeleza unyama huo pia alimzika katika Shamba lake kijana wake huyo ambaye alikuwa anasoma darasa la kwanza katika Shule ya msingi Likweso baada ya kumuweka katika mfuko wa mbolea baada ya Wanafamilia kukataa kumsaidia kuuzika mwili wa marehemu mtoto wake kutokana na kutoridhisha na sababu alizozitoa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Akili Mpwapwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Majira ya usiku wa kuamkia March 5 mwaka huu katika Kijiji hicho baada ya kumfamia Marehemu akiwa amelala na baadae kwenda kuripoti kwa ndugu zake kuwa Mtoto huyo aliugua malaria ghafla usiku wa tukio hilo.

Alisema katika tukio hilo kaka wa marehemu ambaye hakumtaja jina lake alipeleka taarifa kwa ndugu zao na baadae  kwa mtwandaji wa Kijiji hicho Bw. Juma Said ambaye alilipoti uwepo wake katika Kituo kidogo cha polisi cha Masuguru March 8 mwaka huu.

Alisema baada ka kupokea taarifa hizo kituoni hapo nao walipeleka katika kituo cha Polisi Wilaya ya Tunduru ambao paomja na mambo mengine walipeleka Maombi katika mahakama ya wilaya ya tunduru kwa ajili ya kuomba kibali cha kwenda kuufukua mwili wa Marehemu.

Alisema Mtuhumiwa huyo atapelekwa Mahakamani ili sharia iweze kufuata mkondo wake baada aya kukamilika kwa taratibu za uandikaji wa maelezo ya mtuhumiwa huyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Magnga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Dkt.Geofrey  Malawi inaonesha kuwa Chanzo cha Kifo hicho kilitokana na mvunjiko wa Shingo.


Na Steven Chindiye wa demashonews, Tunduru

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com