Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Balaa la Mwaka!!! MKE WA MTU APIGIWA NGOMA BAADA YA KUFUMANIWA AKISALITI NDOA,MME ALIKODI WAPIGA NGOMA,ASHUSHA KIPIGO CHA MBWA MWIZI

Vijana wakipiga ngoma wakati wa fumanizi la Asha.

Mwanadada aliyetambulika kwa jina la Asha baada ya kufumaniwa akisindikizwa na ngoma.

AMA kweli dunia ina mambo na mambo yenyewe ndiyo haya! Katika hali ya kushangaza, mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ramadhan Ally, mkazi wa Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro amewashangaza wengi kufuatia uamuzi wake wa kukodi ngoma ya asili kwa lengo la kwenda kumfumania mkewe aliyejulikana kwa jina moja la Asha. 

 Tukio hilo lililofunga mtaa lilijiri asubuhi ya saa 3:14  Jumatatu iliyopita eneo maarufu kwa jina la Sultani baada ya mwanaume huyo kutonywa kuwa, mke wake alikuwa amelala kwa rafiki yake kipenzi, Abdallah Elias.

 Baadhi ya wananchi waliobahatika kuwasili katika eneo la tukio walishuhudia mwenye mali akiwashushia kichapo kikali ‘wasaliti’ hao ambapo vurugu zikapamba moto.

 Kufuatia hali hiyo, viongozi wa serikali ya mtaa huo waliamua kutoa taarifa kwa Kamanda Mkuu wa Ulinzi wa Jadi Kata ya Mbuyuni, Aidan Mtimbo ambaye alifika eneo la tukio na vijana wake na kuwasomba watuhumiwa hao msobemsobe huku wakisindikizwa na ngoma hiyo hadi Kituo cha Polisi Kata ya Mbuyuni.
 


 Katika hali ya kushangza, nje ya kituo hicho cha polisi baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira walishinikiza watuhumiwa watolewe nje wawafanyie kitumbaya huku baadhi yao wakikipopoa mawe kituo hicho kilichokuwa na askari mmoja aliyevaa nguo za kiraia.

 Baada ya vurugu hizo, afande huyo alipiga simu kituo kikuu cha polisi kuomba msaada ambapo askari wa pikipiki walifika na kuwakodia teksi watuhumiwa hadi kituoni.

 Mwandishi wetu alifanikiwa kuwahoji wahusika wote watatu ambapo mume wa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza kama ifuatavyo:

 “Huyu mwanamke ni malaya sana, kwanza  nimemtoa kwao Matombo (Morogoro) akiwa na watoto wawili na kila mmoja na baba yake.

 “Mimi sikujali hilo, ukipenda bonga penda na ua lake. Miezi mitatu iliyopita aliniambia ana ujauzito wangu, taarifa hizo zilinifurahisha sana. Cha ajabu juzi akaniambia ametoa mimba yangu, nilipomuuliza kwa nini, akasema kwa ujeuri eti hayupo tayari kuzaa na mimi kwa sasa.

 “Nilichukua uamuzi wa kumrudisha kwao, jana usiku napokea taarifa kuwa yuko nyumbani kwa rafiki yangu kipenzi, Abdallah Elias.
 
 

Polisi baada ya kutinga eneo la tukio kuwanusuru watuhumiwa.

“Ndiyo asubuhi nikakodi ngoma na kwenda, niliwakuta wamelala kitandani.”
Kwa upande wake Elias alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema: 

“Huyu mwanamke ni mbaya sana, ametuchanganya mimi na rafiki yangu Dullah, yeye kaja kwangu jana Jumapili akaniambia  amefukuzwa na mumewe hivyo anaomba alale kwangu kesho  yaani leo aende kwao Matombo kumbe alisharudishwa kwao toka juzi.”

 Naye mwanamke huyo alipohojiwa na paparazi wetu alikuwa na haya ya kusema:
“Huyu mwanaume (Ramadhan) hajanioa, kila siku nikimwambia twende kwa wazazi wangu ananipiga danadana. 

Ni kweli nimetoa mimba yake, siko tayari kuzaa naye mtoto nje ya ndoa. Huyu Elias, yeye alionesha nia ya kunioa.”
 

Mume wa Asha, Ramadhan Ally.

 Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samuel Msuya amethibitisha kutokea kwa fumanizi hilo kwenye mtaa wake lakini aliwatupia lawama polisi wa pikipiki kwa kupuuza uongozi wa juu wa kata hiyo ambao kwa kushirikiana na walinzi wa jadi walifanikiwa kuwalinda watuhumiwa wao na kufika salama kwenye kituo cha polisi.

via>>gpl

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com