Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking News!! RACHEL HAULE "RECHO" WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA




Rachel Haule "Recho" enzi za uhai wake
Habari zilizotifikia hivi punde zinasema kuwa Mwigizaji wa bongo movie Rachel Haule "Recho" amefariki dunia


Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. 

Habari zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.

Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana. Kifo hiki kimeleta mshtuko mkubwa kwenye tasnia  ya filamu za kibongo. 

Habari kamili kuhusu tukio hili tutakuletea hivi punde...........
Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Recho.Amina!!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com