Wananchi wa kijiji cha Kibaigwa wamefunga Barabara kuu ya Morogoro kwenda Dodoma usiku huu, kwa madai ya kutaka kupunguzwa Kwa ushuru wa mazao na kuamua kufunga barabara hiyo ili waweze kuonana na uongozi wa juu wa Serikali ili kusikilizwa mahitaji yao ambayo wanadai hayajawahi fanyiwa kazi na viongozi wa Kijiji.
Kinachoendelea hivi sasa ni Jeshi la Polisi likijaribu kuwatawanya wananchi hao kwa kutumia mabomu ya machozi.
Wananchi hao wamejikusanya kuwatawanya kwa wingi katika eneo hilo huku wakiwa wamewasha moto mkubwa ambao umepelekea kuwaka kwa gari moja lililopo kwenye eneo hilo kutokana na kuzuiliwa na wananchi hao huku wakisema hapiti mtu leo hapa.
Magari ya kwenda na kurudi kutoka mikoa ya dodoma na mingine ya kanda ya ziwa yamekwama pande zote mbili za barabara kwa zaidi ya saa sasa .Gari moja LA serikali limeharibiwa na wananchi hao.
Mtandao huu utaendelea kuwapa taarifa kadri zinavyotufikia
via>>michuzi blog