CCM Noma sana!!! TAZAMA JINSI WALIVYOFANYA KUFURU MJI WA ISAKA KAHAMA,TUKIO ZIMA LIKO HAPA ZIARA YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA KHAMIS MGEJA NA WABUNGE WA JIMBO LA MSALALA NA KISHAPU,MAIGE NA NCHAMBI


Viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na mwenyekiti wa ccm  mkoa Ndugu Khamis Mgeja (wa pili kutoka kulia),aliyekuwa ameambatana mbunge wa jimbo la Kishapu mheshimiwa Suleiman Masoud Nchambi(aliyevaa miwani) na mbunge wa Msalala mheshimiwa Ezekiel Maige( wa tatu kutoka kulia)katibu wa siasa na uenezi ccm mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mlimandago wakiwasili katika kijiji na Kata ya Isaka wilayani Kahama jana kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.
Mambo yaliyofanyika katika mji wa Isaka hapo jana ni pamoja na kufungua ofisi ya timu ya mpira wa miguu ya Isaka(Isaka Stars),kukabidhi vifaa mbalimbali kwa kijiwe cha BBC,kukabidhi mifuko 10 ya saruji kutoka ofisi ya ccm mkoa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho lakini piamwenyekiti huyo wa ccm mkoa kuzungumza na viongozi wa ccm kata ya Isaka,pamoja na kufanya harambee kuchangia timu 14 za mpira wa miguu zilizopo katika kata ya Isaka
Wa pili kutoka kulia ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja mara baada ya kukata utepe wakati wa uzinduzi wa ofisi ya timu ya mpira wa miguu  ya Isaka(Isaka Stars) iliyoanzishwa mwaka 2011 ambayo ni miongoni mwa timu zinazofanya vizuri katika wilaya ya Kahama na mkoa wa Shinyanga kwa ujumla.Katika kuipa nguvu timu hiyo pamoja timu zingine 13 za kata ya Isaka,Mbunge wa jimbo la Kishapu aliahidi kutoa mipira miwili kwa kila timu katika kuunga mkono jitihada za mbunge wa jimbo la Msalala  Ezekiel Maige katika sekta ya michezo,na sekta zingine za maendeleoa lakini pia mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya kwa kuhamasisha michezo katika wilaya yake.
Mbunge wa jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga Ezekiel Maige akizungumza wakati wa ufunguzi wa ofisi ya timu ya Isaka(Isaka stars) ambapo katika kuonesha kuwa anaunga mkono michezo katika jimbo lake aliahidi kutoa shilingi milioni moja laki nne kwa timu za mpira wa miguu katika kata ya Isaka katika jimbo lake la Msalala hukua akiahidi kufuatilia mipira 28 iliyotolewa na mbunge wa jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi ambaye ameonesha mfano wa pekee kwa kutembelea jimbo la mbunge mwenzake hali inayoonesha kuwa kiongozi yeyote wa ccm ni kiongozi wa eneo lolote hakuna mipaka kiutendaji
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akizungumza baada ya kufungua rasmi ofisi ya Nyota Football club(Isaka Stars) ambapo alisema suala la michezo lipo katika ilani ya ccm hivyo kilichofanyika ni utekelezaji wa ilani hiyo na kuongeza kuwa michezo mbali na kuwa sehemu ya burudani,mshikamano lakini pia ni ajira.Katika ziara hiyo kulifanyika harambee kuchangia timu hiyo pamoja na zingine ambapo jumla ya shilingi milioni 2,laki5, 55 elfu na 500 zilipatikana 
Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akizungumza mara baada ya kufungua ofisi za timu hiyo.Mgeja alitumia fursa hiyo kuwapongeza wabunge wote wa mkoa wa Shinyanga kuhusu namna wanavyounga mkono michezo kwa kuzisaidia kwa hali na mali timu za mpira mkoa wa Shinyanga mfano Isaka Stars,Stand United,Mwadui FC,Maganzo na zingine kibao hali inayoonesha kuunga mkono jitihada za rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete katika kuinua michezo nchini,Mgeja aliongeza kuwa ni vyema sasa halmashauri zikaanza kutenga bajeti kwa ajili ya michezo
Ziara inaendelea-Mbunge jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga Ezekiel Maige akimkaribisha mwenyekiti wa ccm pamoja na viongozi wengine wa chama katikakatika kijiwe maarufu cha Kahawa cha wakereketwa,katika kijiji cha Isaka kata ya Isaka wilayani Kahama,Kijiwe hiki ni maarufu kwa jina la BBC ukweli na uhakika.

Maige alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kutumia kijiwe hicho kuelimishana kuhusu mambo mazuri yanayofanywa na CCM katika sekta mbalimbali kama michezo,afya,maji,barabara n.k na kuwapuuza wapinzani wanaohubiri kila kukicha kwamba ccm haijafanya chochote cha maana.

Mbunge huyo wa Msalala katika kuunga mkono wajasiriamali wa kijiwe hicho akiwachangia shilingi laki 3 huku akimshukuru mbunge wa Kishapu kwa upendo aliouonesha  kwa wakazi wa Isaka.

Ni katika kijiwe maarufu cha Kahawa cha wakereketwa,katika kijiji cha Isaka kata ya Isaka wilayani Kahama,Kijiwe hiki ni maarufu kwa jina la BBC ukweli na uhakika,ambacho jana Jumapili kimefunguliwa na mbunge wa jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi japokuwa kipo katika jimbo la Msalala.Mbunge huyo mbali na kufungua kijiwe hicho pia amekabidhi viti 14 vya plastiki pamoja meza zake,vikombe,chupa pamoja na vitendea kazi vingine kibao kwa mgahawa huo wa BBC
Shina la wakereketwa kijiwe cha Kahawa cha BBC katika kata ya Isaka wilayani Kahama,ambako mwezi Machi mwaka huu,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja alikabishi runinga kwa ajili ya wajasiriamali hao kupata habari zinazoendelea hapa duniani
Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi ambaye amewahi kuishi Isaka siku za nyuma,akikabidhi viti kwa kijiwe hicho.Kushoto ni mwenyekiti wa BBC Ally Salum Msangi Pajero akipokea kiti,kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja

Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi(mwenye miwani) akikabidhi vifaa muhimu kwa ajili ya wajasiriamali wa kijiwe cha BBC ambapo pamoja na mambo mengine alisema ameamua kutoa zawadi hizo kuonesha upendo kwa wananchi bila ubaguzi wowote huku akitumia fursa hiyo kuiamini ccm na kuwa tayari kukosoa viongozi pale wanapokwenda kinyume na wanavyotaka na kuwaomba wakazi wa Kahama kuendelea kumuunga mkono mbunge wao Ezekiel Maige
Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akiwa ameshikilia moja ya vitendea kazi kwa ajili ya kijiwe cha BBC vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Kishapu
Mwenyekiti wa shina la wakereketwa (Kijiwe cha Kahawa cha  BBC) Ally Salum Msangi Pajero akiwa ameshikilia vitendea kazi vilivyoletwa na mbunge wa Kishapu kupitia ccm Suleiman Nchambi.Pajero alisema kijiwe hicho kimeanzishwa mwezi Januari mwaka 2014 na amewapongeza viongozi hao wa ccm kwa kuwa karibu na wananchi kwa kuwafikia bila kujali matabaka wenye nacho na wasio nacho

Mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Suleiman Nchambi akiwa ameshikilia tikiti maji,baada ya kupewa kama zawadi na wakazi wa Isaka kuonesha furaha yao kuhusu kuja kwake katika kata hiyo

Baada ya Kukabidhi vitendea kazi-Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi,mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja pamoja na mbunge jimbo la Msalala Ezekiel Maige wakinywa kahawa inayopikwa katika kijiwe cha wakereketwa cha BBC ukweli na uhakika katika kata ya Isaka
Ziara inaendelea-Kulia ni mwenyekiti wa kijiji cha Isaka,kata ya Isaka wilayani Kahama, Said Hamad Shanduti akizungumzia kuhusu mradi wa ujenzi wa kituo cha afya unaoendelea katika kijiji hicho,ambapo ziara hiyo ilikuwa neema kwake kwani aliweza kukabidhiwa mifuko 10 ya saruji kutoka ofisi ya ccm mkoa,mbunge Msalala Ezekiel Maige akachangia mifuko 20 ya saruji,mbunge wa Kishapu Nchambi shilingi laki 7 na madereva wa magari yake(50) kila mmoja mfuko mmoja wa saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho afya



Zoezi la kukabidhi mifuko ya saruji kwa uongozi wa serikali ya kijiji cha Isaka unaendelea

Katika kufanikisha ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Isaka,harambee ilifanyika,wadau mbalimbali wa maendeleo wakajitokeza kuchangia chochote,pichani (mbele) ni  Machimu Ndalo maarufu Mwanandalo
mganga wa jadi kutoka kijiji cha Mwakata kata ya Isaka,ambaye pia ni mtemi wa jeshi la jadi sungu sungu kata ya Isaka,ambaye pia mlezi wa jumuiya ya wazazi ccm wilaya ya Kahama,alichangia mifuko 5 ya saruji.Katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha afya mifuko 137 ya saruji ilipatikana pamoja na shilingi laki 8 na elfu 50. 
 Baada ya zoezi la kukabidhi mifuko kukamilika mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga alifanya mkutano wa ndani na viongozi wa ccm kata ya Isaka na baadaye kufanya harambee ya kuchangia timu za mpira wa miguu katika kata hiyo ambapo jumla ya shilingi milioni 2,laki 5,55 elfu na 500 zilipatikana pamoja mipira 28.

Picha zote na Kadama  Malunde  wa malunde1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم