Mwanamke huyo aliandika kwenye Facebook kuwa alikuwa anaenda kumtembelea rafiki yake kabla ya kuuawa |
Polisi nchini Japan wanachunguza kisa cha kushangaza ambapo maiti ya mwanamke aliyeuawa ilitumwa kutoka Osaka hadi Tokyo kwa njia ya posta.
Inaaminika mwanamke huyo, Rika Okada, alichomwa kisu na mwili wake kuwekwa ndani ya sanduku ambalo lilitiwa kibandiko na karatasi iliyosema kuwa sanduku hilo lilikuwa limemeba mwanasesere.
Sanduku hilo, liligunduliwa likiwa katika sehemu ya kuhifadhi vitu katika kituo cha posta.
Polisi wanasema kuwa sehemu ambako sanduku hilo lilipatikana limewekwa, lilikuwa limekodishwa kwa kutumia kadi ya benki ya mwanamke huyo.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alitoweka tangu mwishoni mwa mwezi Machi, alipotuma ujumbe wa mwisho kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba alikuwa anaenda kukutana na rafiki yake wa muda mrefu ambaye alikuwa hajamuona kwa miaka mingi.
via>>bbc
Social Plugin