Wananchi wakisaidia katika uvutaji wa gari hiyo iliyokuwa ikivutwa na Lori kuitoa mtaroni |
Ajali hiyo imetokea leo majira na saa nane mchana katika barabara kuu iendayo nchini Ruanda kwenye eneo la KTM mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Imeelezwa kuwa gari hiyo kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilipasuka tairi moja ya mbele na kupelekea kuacha njia na kupinduka mtaroni, lakini hata hivyo hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika ajali hiyo.